loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Minziro, Waziri wang’ara

MSHAMBULIAJI wa Mbao FC ya Mwanza, Waziri Junior amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Julai wa Ligi Kuu msimu wa 2019/20 huku kocha wa kikosi hicho, Fred Felix Minziro akichaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi huo.

Waziri na Minziro wametwaa tuzo hizo baada ya kuwashinda wenzao walioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa na Kamati ya tuzo zinazotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

“Kwa mwezi huo wa Julai, Mbao ilicheza michezo sita, ikashinda michezo mitano na kupata sare moja na Waziri akiwa sehemu kubwa ya mafanikio hayo kwa kuifungia timu yake mabao matano na kutoa pasi moja ya mwisho,” ilisema taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari.

Taarifa hiyo ilisema Waziri amewashinda Peter Mapunda wa Mbeya City na Obrey Chirwa wa Azam FC alioingia nao fainali.

Mapunda aliisaidia timu yake kushinda michezo minne kati ya sita waliyocheza akifunga mabao matatu na kutoa pasi mbili za mwisho na Chirwa akifunga mabao manne yaliyoisaidia Azam kushinda michezo mitatu na kupata sare mbili katika michezo sita.

Kwa upande wa Minziro, amewashinda Amri Said wa Mbeya City na Aristica Cioaba wa Azam, ambapo Minziro aliiongoza Mbao kushinda michezo mitano kati ya sita waliyocheza mwezi huo na kupata sare moja.

Amri Saidi aliiongoza Mbeya City kushinda michezo minne kati ya sita huku Cioaba akiiongoza Azam kushinda michezo mitatu, sare mbili na kupoteza mmoja.

MWIGIZAJI maarufu wa tamthilia ya Karma, Wema Sepetu amewaomba radhi ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi