loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wagombea 4 Viti Maalumu UVCCM watupwa nje

KAMATI ya Utelekezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM) Taifa, imebaini wagombea wanne wa Ubunge Viti Maalumu wamevunja kanuni ya jumuiya hiyo.

Kutokana na kuvunja kanuni, jumuiya hiyo imechukua uamuzi wa kuwachukua washindi wa pili wa kura za maoni kwenye mikoa husika ambao wamekidhi vigezo.

Uamuzi wa jumuiya umesemwa na Kaimu Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UV-CCM Taifa, Leonard Singo jijini hapa jana.  

Singo alikuwa akizungumzia maandalizi ya Mkutano Maalumu wa Baraza la UV-CCM Taifa ambao unafanyika leo jijini hapa kwa ajili ya kuchagua viongozi hao kupitia kundi la vijana.

Hata hivyo Singo, hakutaka kuweka wazi majina ya wagombea hao na kudai kuwa kwa sasa ni siri ya vikao.

Alisema mchakato huo umekwenda vizuri kwa kuzingatia kanuni na miongozo ya Jumuiya hiyo.

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

UDASA yataka wagombea waache matusi

dakika 13 zilizopita  Ikunda Erick

JUMUIYA ya ...

Hazina yataka Shirika la Posta wapunguze matumizi

dakika 14 zilizopita Anastazia Anyimike, Dodoma

MSAJILI ...

Andengenye: Wahitimu JKT someni kozi zenye soko

dakika 44 zilizopita Fadhili Abdallah, Kigoma

MKUU wa Mkoa Kigoma, ...