loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga SC, Namungo zamgombea Blaise

SIKU moja baada ya Yanga kudaiwa kuanza mazungumzo na mchezaji Bigrimana Blaise wakihitaji saini yake, klabu ya Namungo FC imesema nyota huyo muda wowote kuanzia sasa anatarajia kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Namungo wamelazimika kutoa ufafanuzi baada ya kuzagaa kwa kwa taarifa kuwa tayari Yanga wameanza kufanya mazungumzo na mchezaji huyo wakati timu yake ikidai Blaise ameonesha nia ya kubaki kwenye kikosi hicho.

Akizungumza kutoka Ruangwa, Lindi Mwenyekiti wa Namungo, Hassan Zidadu alisema Blaise pamoja na wachezaji wengine tegemeo ambao mikataba yao inaelekea ukingoni wanaendelea kufanya nao mazungumzo ya kuwabakisha, ambapo hadi sasa wamefikia asilimia 95 kuwabakisha .

‘’Blaise tumeshafanya naye mazungumzo na muda wowote anatarajia kusaini mkataba wa kuendelea kuitumikia timu yetu, sio huyo tu kuna wachezaji wengine kama Reliants Lusajo tunafanya hivyo kuona wanabaki kuisaidia timu,”alisema Zidadu.

Alisema wanatambua soka ni ajira kwa sasa na wachezaji wanatafuta maslahi kwa lengo la kuboresha Maisha yao, hivyo wanatambua hilo na mazungumzo wanayoyafanya na nyota wao yanazingatia mahitaji ya pande zote .

Blaise imeitumikia Namungo kwa msimu ulipita kwa mafanikio kwa kuifungia timu hiyo mabao 13 kwenye mechi za Ligi na kuifikisha kwenye hatua ya mafainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Federation Cup na kufanikiwa kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi kimataifa.

Hata hivyo, Ofisa Muhamasishaji wa Yanga, Antonio Mugaz alisema jana kuwa klabu yao haina mpango na mchezaji huyo na hizo taarifa nazo wanazisikia na kuziona katika mitandao ya kijamii tu.

Alisema mashabiki watulie kama kuna mchezaji wanataka kumsajili, watamtangaza rasmi.

MWIGIZAJI maarufu wa tamthilia ya Karma, Wema Sepetu amewaomba radhi ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi