loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbeya City yapata funzo

TIMU ya soka ya Mbeya City imesema ugumu waliopitia msimu uliopita wa Ligi Kuu umewapa funzo kubwa, hivyo hawataki yajirudie tena msimu ujao.

Mbeya City imenusurika kushuka daraja baada ya kumaliza ligi katika nafasi za chini na kucheza mchezo wa mtoano dhidi ya Geita Gold na kushinda, ambapo uliwapa nafasi ya kubaki kwa ajili ya msimu ujao.

Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe aliliambia gazeti hili kuwa kile walichokipitia hadi kumaliza ligi katika nafasi za chini hawataki tena kitokee.

“Msimu uliopita kwa kweli tulipata wakati mgumu mno, tunashukuru kwamba tumebaki na sasa tunapitia ripoti ya kocha wetu kujua kile ambacho amekipendekeza kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya,”alisema.

Kimbe alisema anaamini timu hiyo itarudi kivingine kwani wanatarajia kufanya usajili ili kurudi katika kasi mpya.

Alisema mabadiliko watakayoyafanya anaamini yatakuwa yenye uhai kwa timu hiyo kurudi kwa nguvu mpya na ushindani kama ilivyotokea miaka ya huko nyuma.

Mbeya City ni moja ya timu zilizokuwa na ushindani mkubwa msimu wa 2013/2014 na 2014/2015 baada ya kumaliza ligi katika nafasi za juu  lakini kadiri miaka ilivyosogea kikosi chao kilianza kufumuliwa na timu nyingine na kujikuta kiwango chao kikizidi kushuka.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine