loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

…Msumbiji yakanusha kuhusika na mlipuko Beirut

MAMLAKA ya bandari nchini Msumbiji imekanusha madai kwamba meli yake ilikuwa imebeba mzigo uliosababisha mlipuko wa Beirut.

Meli hiyo ambayo ilikuwa inatokea bandari ya Beira, nchini Msumbiji inadaiwa kuwa ilishusha mzigo Beirut na shehena ya mzigo ambao ulihifadhiwa katika ghala ya bandari.

"Mamlaka ya bandari haikuwa inajua kuwa meli ya Mv Rhosus iliacha mzigo katika bandari ya Beira," ilieleza mamlaka ya bandari ya Beira.

Inasema hakukuwa na tangazo la kuwasili kwa meli bandarini hapo ndani ya siku saba mpaka 15.

Lakini maofisa wa bandari ambao hawakutaka majina yao yatajwe, walisema ingawa meli hiyo ilikuwa imewasili katika bandari ya Beira, lakini safari yake ilikuwa haipaswi kuishia Msumbiji bali Zimbabwe au Zambia, kwa sababu ilikuwa imebeba kemikali inayotumika kutengeneza mlipuko kwa ajili ya sekta ya migodi.

Mamlaka ya bandari inayofuatilia mienendo ya meli, ilisema kuwa vyombo vya majini vinavyopeperusha bendera ya Moldoval viliwasili Beirut tangu Novemba 20, mwaka 2013 na havijawahi kuondoka.

 

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: MAPUTO, Msumbiji

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi