loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Trump azuia matumizi ya tiktok na WeChat

RAIS wa Marekani Donald Trump amesaini maagizo ya utendaji yaliyolenga kuzuia matumizi ya mitandao ya kijamii ya Tiktok na WeChat ambayo ni programu za China.

Kupitia maagizo hayo, kampuni za Marekani lazima zisitishe kufanya biashara na kampuni zenye progamu hizo ndani ya siku 45. Kwa mujibu wa Trump uamuzi huo umechukuliwa kwa sababu za kiusalama.

Hii inachukuliwa na wachambuzi wa mambo ya kisiasa kwamba ni hatua kubwa katika msimamo unaozihusu nchi hizo mbili Marekani na China katika teknolojia ya dunia.

Aidha, uamuzi huo wa Marekani umekuja wakati kampuni ya Microsoft ikiwa kwenye mazungumzo ya kununua mtandao wa Tiktok kabla ya siku ya mwisho ya kusitisha uhusiano wa kibiashara iliyowekwa na Trump ambayo ni Septemba 15, mwaka huu.

Uamuzi huo dhidi ya mtandao wa Tiktok ambayo ni wa kutuma video fupi unaomilikiwa na kampuni ya China ya ByteDance na mtandao wa ujumbe mfupi ya WeChat inayomilikiwa na Tencent Conglomerate ni hatua yamwisho ya uongozi wa Trump dhidi ya China.

Hata hivyo, kwa mujibu wa wachambuzi uamuzi huo wa Trump unaweza kupingwa kisheria.

Mapema juzi, Marekani ilitanganza mapendekezo ambayo kampuni za China katika Soko la Hisa la nchi hiyo zinatakiwa kuyatekeleza isipokuwa kama walitoa wasimamizi na akaunti zao zilizokaguliwa.

Katika maamuzi hayo, Rais Trump alisema lazima hatua muhimu zichukuliwe katika kushughulikia dharura ya kitaifa kuhusu teknolojia na habari ya mawasiliano na mlolongo wa usambazaji wa huduma.

“Kusambaa hapa nchini kwetu programu za simu zinazomilikiwa na kampuni za China kunaendelea kuwa tushio kwa usalama wetu kama taifa, sera za kigeni na uchumi wa taifa letu,” alisisitiza Trump.

JUMUIYA ya Nchi za Afrika, Carribean na Pacifi c (OACPS) ...

foto
Mwandishi: WASHINGTON, Marekani

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi