loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maandamano yaibuka Beirut kuipinga serikali

WAANDAMANAJI katika mji wa Beirut nchini Lebanon waliokuwa wakiipinga serikali walijikuta katika wakati mgumu baada ya kukabiliana na vikosi vya usalama.

Maofisa wa usalama walirusha mabomu ya machozi kwa kundi la waandamanaji hao waliokuwa karibu na Bunge.

Waandamanaji hao walikasirishwa na mlipuko uliotokea Jumanne, ambapo maofisa walisema ulisababishwa na tani 2,750 za kemikali ya ammonium nitrate ambazo zimekuwa zikihifadhiwa kwa njia isiyo sahihi tangu mwaka 2013.

Raia wengi wa Lebanon walisema upuuzaji wa serikali ndio chanzo cha mlipuko huo, uliosababisha vifo vya watu takribani 137 na kujeruhi wengine 5,000.

Mlipuko huo uliharibu eneo zima la mji huo huku nyumba na biashara zikiharibiwa kabisa.

Shirika la habari linalomilikiwa na serikali limesema kwamba watu 16 wametiwa mbaroni kama sehemu ya uchunguzi uliotangazwa na serikali wiki hii.

Mbunge Marwan Hamadeh alijiuzulu Jumatano, huku balozi wa Lebanon nchini Jordan, Tracy Chamoun akijiuzulu Alhamisi, na kusema kwamba janga hilo limeonesha haja ya mabadiliko katika uongozi.

Mapema Alhamisi, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pia alitembelea mji huo na kusema Lebanon inahitaji mabadiliko ya kina katika ngazi ya mamlaka.

Pia alitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wa kimataifa kuhusu janga hilo.

JUMUIYA ya Nchi za Afrika, Carribean na Pacifi c (OACPS) ...

foto
Mwandishi: BEIRUT, Lebanon

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi