loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Vyama vya siasa leteni viongozi wenye sifa

WAKATI zikiwa zimebaki siku chake kufikia hatua ya vyama vya siasa nchini kuanza kampeni, kwa sasa takribani vyama vyote bado viko katika hatua ya kuchagua wagombea watakaoviwakilisha vyama hivyo kwenye nafasi za ubunge, udiwani na uwakilishi.

Katika nafasi ya urais, tayari baadhi ya vyama vimekamilisha hatua hiyo ikiwemo walioteuliwa kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania nafasi hiyo kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliyofungua dirisha hilo tangu Agosti 5 na litafungwa Agosti 25, mwaka huu.

Ni wazi kuwa bado baadhi ya vyama vinaendelea na mchakato wa mchujo wa wagombea wake kwa ngazi ya vikao vya juu zaidi ili kuweka wagombea wenye sifa za kutosha kuwakilisha vyama hivyo kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Mwaka huu uchaguzi tofauti na miaka mingine, idadi kubwa ya wanachama imejitokeza kuomba ridhaa kuwakilisha vyama vyao kwenye nafasi za ubunge, udiwani, uwakilishi na hata urais.

Ikumbukwe kuwa viongozi bora ni wale walio tayari kujitolea kwa ajili ya wananchi wanaowatumikia, wanaochukia rushwa, urasimu na wasioweka mbele maslahi yao binafsi lakini pia wenye maono mapana juu ya dhana nzima ya maendeleo na maisha bora ya watu wanaowatumikia.

Ili kuwapata viongozi angalau wenye sifa chache kati ya hizo ni vyema kuangalia mienendo ya waliojitokeza kutangaza nia hasa katika harakati zao za kutaka kupata uongozi huo.

Pongezi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuamua kuwashangaza na kuwashikisha adabu viongozi waliotumia njia za udanganyifu ikiwemo vitendo vya rushwa ili kupata ridhaa ya kuwakilisha chama hicho kwenye uchaguzi.

Ni wazi kuwa vyama vyote vina wajibu wa kuhakikisha vinaweka wagombea wanaokidhi matakwa na mahitaji ya watanzania katika suala zima la uongozi kwa maana ya kupata viongozi bora na si bora viongozi.

KAMPENI za uchaguzi kwa ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi