loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Temesa yaiumiza kichwa serikali

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango( pichani) amekerwa na kusema Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA),ni moja ya taasisi zenye matatizo makubwa ndani ya serikali kutokana na kutumia fedha nyingi kufanya matengenezo na ununuzi wa vipuri vya magari ya serikali.

Dk Mpango alitoa kauli hiyo jana wakati akitembelea mabanda ya Wizara hiyo katika maonesho ya wakulima, wafugaji na wavuvi yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabidi mkoani Simiyu.

Akiwa kwenye banda la Mifumo ya Fedha, Dk Mpango alipewa maelekezo ya jinsi kitengo hicho kinavyofanya kazi ya kudhibiti mifumo ya malipo serikalini ambapo aliambiwa hivi sasa udhibiti wa matumizi ya fedha umeboreka maradufu.

Hata hivyo wakati akipewa maelekezo hayo alisema ni vyema kitengo hicho kikaangalia kama kuna uwezekano wa kuwa na mfumo utakaorekebisha utaratibu wa malipo ya TEMESA kwa sababu fedha zinazotumika kwenye matengenezo na ununuzi wa vipuri vya magari ya serikali ni nyingi.

“Kama kuna taasisi ya serikali inayoumiza kichwa na yenye shida ni TEMESA, kuna shida huko kama kuna mfumo utaweza kurekebisha itatusaidia sana,bei za matengenezo na ununuzi wa vipuri vya magari ya serikalini ni kubwa sana, ingewezekana tungefukuza wote huku Temesa ,tuanze moja ni vizuri zaidi,” alisema.

Hata hivyo alizigeukia pia halmashauri nchini na kusema bado kuna ubadhirifu mkubwa unaofanywa kwenye matumizi ya fedha za serikali ambao miradi inayotekelezwa huku haiendani na thamani ya fedha iliyotumika.

“Niwatake sasa nyie watu wa mifumo boresheni mfumo wa fedha hasa kwenye halmashauri kwa sababu wana matumizi yasiyoendana na thamani ya fedha, fuatilieni, nendeni huko mtayaona maana bado serikali ‘inapigwa’,” alisema Waziri Mpango.

Akiwa katika banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Waziri Mpango aliwapongeza kwa kazi nzuri wanayoendelea kufanya ya udhibiti na kuwataka watoe elimu zaidi kwa umma kuhusu matumizi bora ya fedha za serikali ili yaendane na thamani halisi ya fedha iliyotolewa.

JAMII imehadharishwa dhidi ya tabia ya ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick, Bariadi

Post your comments

Habari Nyingine