loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwarobaini wa pembejeo feki wapatikana

MWAROBAINI wa kudhibiti pembejeo feki sokoni umepatikana baada ya kuzinduliwa kwa huduma maalumu ya kuhakiki ubora wa pembejeo hizo uitwao T-Hakiki .

Akizindua huduma hiyo juzi katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu kwenye maonesho ya wakulima, wafugaji na wavuvi Waziri wa Kilimo ,Japhet Hasunga alisema huduma hiyo itamaliza tatizo la uwepo wa pembejeo feki za kilimo nchini.

Huduma hiyo imebuniwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu Ukanda wa Tropiki (TPRI),Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu nchini (TOSCI) na Kampuni ya Quincewood.

Hasunga alisema wakati Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akizindua maonesho hayo wiki iliyopita aliagiza wizara hiyo kushughulikia kasoro zilizopo katika upatikanaji wa pembejeo hasa kwenye mbegu na viuatilifu ili kuwasaidia wakulima waweze kutumia pembejeo bora na kuleta tija kwenye uzalishaji.

Akizungumzia huduma hiyo mpya, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba alisema kwa ushirikiano huo wamebuni mbinu hiyo mpya ya kukomesha uuzaji wa pembejeo feki kwa wakulima.

“Huduma hii ni mpya inaitwa T-Hakiki ni mfumo wa njia ya simu ambayo mkulima anachukua simu yake ya mkononi anabofya *148*52# kisha anaingiza namba za siri zilizo kwenye vifungashio vya mbegu au chupa za viuatilifu alivyonunua kisha anabonyeza ok na kumletea maelekezo na kumpa majibu kama alichonunua ni sahihi au bandia,” alisema Kindamba.

Alisema baada ya kuhakiki na kupata majibu kama yakimletea ni feki kwenye chupa ya dawa au mfuko wa mbegu aliyonunua kuna namba za kupiga bure ambazo ni 0800110031 kutoa taarifa kwa ajili ya hatua zaidi.

Kindamba alisema huduma hiyo sio tu kwa mtandao wa TTCL bali unapatikana kwenye mitandao yote ya simu na kusema hiyo ni njia sahihi ya kudhibiti pembejeo feki sokoni zinazowaletea changamoto wakulima.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPRI, Margaret Mollel alisema viuatilifu vyote vinavyoingia nchini ni lazima vikaguliwe na kuidhinishwa na taasisi hiyo ili kuhakikisha wakulima wanatumia pembejeo sahihi.

Hata hivyo alisema pamoja na wao kuhakiki bado kuna baadhi ya wafanyabiashara wachache wasio waaminifu wanaoingiza pembejeo feki sokoni kwa njia za panya na kuzichanganya na zile sahihi hivyo kuwa vigumu kwa wakulima kubaini.

SERIKALI imezindua Mpango Mkuu ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick, Bariadi

Post your comments

Habari Nyingine