loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yatoa miezi sita kumaliza vifo vya wajawazito

MGANGA Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi ameagiza ndani ya miezi sita Waganga Wakuu wote wa mikoa, Waganga Wakuu wa Wilaya na Waganga wafawidhi wa hospitali zote nchini kuongeza kasi katika kupunguza zaidi vifo vya mama na mtoto kwa kuboresha huduma na usimamizi katika maeneo yao.

Mganga Mkuu wa Serikali ametoa agizo hilo leo wakati wakati akiongea na Watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mawenzi-Kilimanjaro kwenye ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma na ujenzi wa miundombinu ya afya katika Mkoa huo.

“Waganga Wakuu wote wa Mikoa, Wilaya pamoja na Waganga wafawidhi wa Hospitali zote mlifanyie kazi hili suala la kupunguza zaidi vifo vya akina mama wajawazito, nawapa miezi mitatu hadi sita, nione hali ya vifo vinashuka zaidi kila mkoa, na Wilaya.

“ Waganga wafawidhi wa Hospitali zote za kanda na wilaya, itakapofika miezi sita nitafanya ufuatiliaji kwa kushirikiana na TAMISEMI, Kiongozi atakaeshindwa tutafanya mabadiliko” amesema

Prof. Makubi amesema kuwa, vifo vya akina mama wajawazito na mtoto vinaweza kuisha kabisa nchini kama kutakuwa na uwajibikaji na kujitoa kwa kila mtu kwa nafasi yake, ikiwemo uratibu mzuri baina ya watoa huduma za afya ili kuondoa ucheleweshaji wa kupata huduma kwa mama wajawazito, huku akisisitiza kuzitumia Hospitali za kanda kubadilishana ujuzi na hospitali za ngazi ya chini, na utambuzi wa viashiria vibaya kwa mjamzito wakati wa mahudhurio kliniki.

“Kuna njia nyingi mnaweza kutumia ili kushinda hili, ikiwemo kuwawezesha Wataalamu ngazi za chini kuwa na uwezo wa kuzuia hiyo shida, kutoa mafunzo kwa kutumia hospitali za kanda tulizonazo, utambuzi wa viashiria vibaya ambavyo anakuwa navyo mjamzito wakati wa kliniki na uratibu mzuri ili kuondoa ucheleweshaji” amesema

 Prof. Makubi amesisitiza, katika kuelekea zoezi hilo, ni muhimu kuhakikisha utoaji takwimu zilizo sahihi zitakazosaidia kuleta mabadiliko kwa kufanya maboresho katika maeneo mbali mbali ya utoaji huduma.

Takwimu za Serikali za mwaka 2016 zinaonyesha kuwa vifo vya mama wajawazito ni 556 kila mwaka kati ya vizazi hai 100,000.

JAMII imehadharishwa dhidi ya tabia ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine