loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Agricom Tanzania yapongezwa kusaidia kuinua Kilimo

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Kampuni ya Agricom Tanzania kwa kuwezesha upatikanaji wa zana mbalimbali za kilimo yakiwemo matrekta, mashine za kuchakata mazao hapa nchini.

“Agricom Tanzania inafanya kazi nzuri ya kuiinua sekta ya kilimo kwa kuhakikisha zana za kilimo zinapatikana kwa wakati nchini pamoja na kutoa mafunzo kwa wakulima na wadau katika sekta ya kilimo,” alisema.

Akizungumza alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu juzi kabla ya kufunga Maonesho ya Wakulima na Wafugaji maarufu Nanenane, Waziri Mkuu alisema Agricom Tanzania ni mfano mzuri mwa kampuni zinazotoa mchango mzuri kwenye sekta ya kilimo.

Majaliwa alisema kuwepo na kampuni za kitanzani kama Agricom Tanzania ni mfano nzuri wa kuwepo kwa sekta binafsi imara yenye uthubutu katika kuchangamkia fursa zilizopo hapa nchini kikubwa zaidi kuendelea kujenga mazingira bora ya kufanya biashara na kuvutia uwekezaji.

Aliongezea kuwa kujenga uchumi wa viwanda nchini kunategemea zaidi upatikanaji wa malighafi ambazo zinatokana na mazao, ufugaji na uvuvi hivyo ni muhimu kuhimiza uzalishaji katika sekta hizo.

Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka wakulima kutumia zana za kisasa zinazopatikana hapa nchini ili kufanya kilimo chenye tija ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo,uvuvi na ufugaji na kupelekea uhakika wa ziada ya chakula.

Alisema sekta ya kilimo chini inachangia asilimia 65 ya malighafi za viwanda na hivyo tukiendelea kutumia vifaa vya kisasa vya kilimo ili kuendelea kufanya uzalishaji wenye tija.

“Sekta ya kilimo,uvuvi na mifugo inatengeneza ajira kwa asilimia 70 hivyo ni jukumu la kila mdau kuhakikisha mazingira yanakuwa wezeshi katika kuinua sekta nchini,” alisema Majaliwa Kwa upande wake Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema wizara yake inaendelea kushirikiana na sekta binafsi ili kuinua kilimo nchini.

“Mpaka sasa tuna uhakika wa ziada ya chakula kwa mwaka hii ni kutokana na kazi nzuri inyofanywa na wakulima katika kuongeza tija ya uzalishaji,”alisema.

SERIKALI imezindua Mpango Mkuu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Bariadi

Post your comments

Habari Nyingine