loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanawake watakiwa kutosubiri kuwezeshwa

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, amewataka wanawake nchini kuondokana na utamaduni wa kusubiri kuwezeshwa katika masuala mbalimbali ya maendeleo, badala yake wapambane kwani wanaweza kujikwamua kiuchumi.

Mkuu huyo wa mkoa alitoa changamoto hiyo wakati wa mkutano mkuu wa saba mwaka wa wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu Tanzania (THTU) wa kujadili changomoto mbalimbali wanazokutana nazo katika taasisi za elimu ya juu, mjini Mtwara hivi karibuni.

“Ombi langu kwenu akinamama, muondokane na tabia ya kupenda kulialia kutaka kuwezeshwa, badala yake mpambane mkijua wanawake mnaweza kutokana na nafasi yenu katika jamii na mjipange kumaliza vitendo vya ukandamizaji katika maeneo ya vyuo, tunachotaka ni kuona wanazalishwa wanawake wazuri kwenye maeneo hayo,” alisema.

“Kwa kile kidogo mnachokipata muwekeze katika uchumi wa kati, nchi sasa imeingia katika uchumi ambao umetokana na kazi ndogo ndogo za mikono zinazotokana na akinamama,” alisema.

Mwenyekiti wa kamati ya wanawake ya THTU, Salma Fundi, alisema wanawake wakielimika na jamiii inaelimika. “Kumuelimisha mwanamke ni sawa na kuelimisha jamii mzima,” alisema.

Kaimu Katibu wa kamati hiyo, Roselyne Mathew, katika taarifa alisema THTU inatambua na kuuenzi mchango mkubwa unaofanywa na serikali hasa kwa kujali maslahi mapana ya mfanyakazi.MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, amewataka wanawake nchini kuondokana na utamaduni wa kusubiri kuwezeshwa katika masuala mbalimbali ya maendeleo, badala yake wapambane kwani wanaweza kujikwamua kiuchumi.

Mkuu huyo wa mkoa alitoa changamoto hiyo wakati wa mkutano mkuu wa saba mwaka wa wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu Tanzania (THTU) wa kujadili changomoto mbalimbali wanazokutana nazo katika taasisi za elimu ya juu, mjini Mtwara hivi karibuni.

“Ombi langu kwenu akinamama, muondokane na tabia ya kupenda kulialia kutaka kuwezeshwa, badala yake mpambane mkijua wanawake mnaweza kutokana na nafasi yenu katika jamii na mjipange kumaliza vitendo vya ukandamizaji katika maeneo ya vyuo, tunachotaka ni kuona wanazalishwa wanawake wazuri kwenye maeneo hayo,” alisema.

“Kwa kile kidogo mnachokipata muwekeze katika uchumi wa kati, nchi sasa imeingia katika uchumi ambao umetokana na kazi ndogo ndogo za mikono zinazotokana na akinamama,” alisema.

Mwenyekiti wa kamati ya wanawake ya THTU, Salma Fundi, alisema wanawake wakielimika na jamiii inaelimika.

“Kumuelimisha mwanamke ni sawa na kuelimisha jamii mzima,” alisema. Kaimu Katibu wa kamati hiyo, Roselyne Mathew, katika taarifa alisema THTU inatambua na kuuenzi mchango mkubwa unaofanywa na serikali hasa kwa kujali maslahi mapana ya mfanyakazi.

JAMII imehadharishwa dhidi ya tabia ya ...

foto
Mwandishi: Sijawa Omary, Mtwara

Post your comments

Habari Nyingine