loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Washauriwa kupima udongo kujua mahitaji

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Raphael Chibunda amesema tatizo kubwa la Tanzania ni kutokuwa na takwimu sahihi kuhusu ubora wa udongo, matokeo yake wakulima wamekuwa wakinunua mbolea kwa bei kubwa bila kujua uhakika wake.

Chibunda alisema hayo katika banda la chuo hicho lililopo katika Maonyesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

Alisema wakulima wengi wananunua mbolea hiyo na kwa kuwa hawajapima udongo wa sehemu wanayotaka kuilima wanakuwa hawana uhakika kama mbolea hiyo ndiyo inayotakiwa kwenye eneo hilo.

Alisema kutokana na changamoto hiyo, SUA imefika katika maonesho hayo na maabara inayotembea ya kupima udongo ili wakulima waweze kupata huduma hiyo katika maonesho hayo.

Kwa upande mwingine alisema chuo hicho kina maktaba ya taifa ya kilimo ambayo inatumiwa na wanafunzi pamoja na wadau wengine kwenye kitengo kijulikanacho kama maktaba ya mkulima.

Naye Mhadhiri kutoka SUA, Philbert Ninyondi alisema kimeanzishwa kitendo maalum katika maktaba ya Taifa ya Sokoine ya kilimo ambacho kazi yake ni kumhudumia mkulima kwa kutumia App hiyo ambayo mkulima mwenye simu janja anaweza kupata taarifa moja kwa moja kutoka kwenye maktaba ambazo zinamwezesha kutumia taarifa za utafiti.

“Pamoja na kutengeneza hii App bado tunafahamu kuna wakulima Tanzania ambao hawana simu janja hivyo wanaangalia namna gani wataweka jukwaa ambalo mkulima ataweza kutumia ile simu yake ya kawaida kupata ujumbe lakini pia kuuliza kitu na kujibiwa,” alisema.

SERIKALI imezindua Mpango Mkuu ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi, Bariadi

Post your comments

Habari Nyingine