loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kampeni kukamata viuatilifu bandia yapamba moto

KATIKA kuhakikisha wakulima, wafugaji na wavuvi wanatumia pembejeo na zana bora za kilimo, Tume ya Ushindani nchini(FCC),imesema kwa ushirikiano na Taasisi ya Utafi ti wa Viuatilifu Ukanda wa Tropiki (TPRI),wamefanikiwa kukamata viuatilifu bandia vilivyoingizwa sokoni ambavyo vinasababisha kuleta matokeo duni.

Akizungumza kwenye maonesho ya wakulima, wafugaji na wavuvi yanayomalizika leo, Mkuu wa FCC, John Mduma alisema katika kipindi cha miaka mitano, tume hiyo imefanikiwa kufanya mengi ikiwa ni pamoja na kukamata viuatilifu hivyo ambavyo vingeharibu matarajio ya wakulima.

Akizungumzia viuatilifu hivyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPRI, Margaret Mollel alisema kwa kushirikiana na tume hiyo wamekuwa wakifanya kaguzi mara kwa mara na kufanikiwa kukamata viuatilifu bandia ambavyo huviteketeza.

Alisema kwa mwaka 2019 walifanikiwa kusajili viuatilifu vipya 66 na katika maonesho hayo kulizinduliwa huduma ya T-HAKIKA ambayo itaanza kutumika kukomesha uuzaji wa pembejeo feki ikiwemo viuatilifu.

Akizungumzia udhibiti wa bidhaa bandia kwa ujumla,Mduma alisema FCC katika kipindi cha miaka mitano sasa wamefanikiwa kukagua jumla ya makasha 29,529 ambapo kati ya hizo 987 yalibainika kuwa na bidhaa bandia.

“Kwa miaka mitano sasa tumefanikiwa kukagua makasha 29,529 ya bidhaa na kati ya hayo tulibaini makasha 987 yalikuwa na bidhaa bandia huku zikiwa na alama za kughushi,”alisema Mduma.

Alisema uingizaji wa bidhaa bandia vikiwemo viuatilifu na pembejeo kwa njia za panya au zile za kawaida unaathiri uchumi na kuleta hasara kwa wakulima,wafugaji na wavuvi ambao hupoteza malengo yao kwa kuwa walichotarajia hakikutimia.

“Mkulima akinunua viuatilifu bandia bila kujua anaharibu malengo la shamba lake kwa maana wadudu wataendelea kushambulia mazao na kama ni dawa ya mifugo haitatibu ugonjwa hivyo mifugo hupoteza maisha na kuleta hasara kwa mfugaji,”alisema Mduma.

JAMII imehadharishwa dhidi ya tabia ya ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick, Bariadi

Post your comments

Habari Nyingine