loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Walemavu wataka serikali kubana wazazi wanaofungia watoto

WANAFUNZI wenye ulemavu wanaosoma shule za msingi mkoani Dodoma wameiomba serikali kutowafumbia macho wazazi na walezi wanaowanyima haki za msingi watoto wao kwa kuwafi cha majumbani.

Mwanafunzi Deo Kasimbu wa Shule ya Msingi ya Nkuhungu, alisema hayo juzi kwenye hafla fupi ya kupokea misaada mbalimbali ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona kwa ajili ya watoto wenye ulemavu iliyotolewa na mradi wa Elimu Jumuishi kitengo cha kanisa la FPCT wilaya ya Dodoma na Bahi.

Akizungumza kwa niaba ya watoto wenye ulemavu, ameiomba serikali kuhakikisha wale wote wanaowanyima haki za msingi, kisheria ikiwemo kwa kuwaficha majumbani, unyanyasaji na unyanyapaa wasifumbiwe macho bali wachukuliwe hatua kali wanapobainika.

Alisema bado kuna changamoto nyingi kwa watoto wenye ulemavu kutokana na tabia ya kufichwa majumbani kwa imani kuwa ni mkosi, badala ya kupelekwa shule ili na wao waweze kupatiwa haki zao za msingi kama vile elimu na afya.

“Jamii lazima itambue kuwa kitendo cha kuwaficha majumbani watoto wenye ulemavu, ni kuongeza umasikini zaidi kwenye familia husika tofauti na wangepelekwa shuleni na kuweza kupata elimu na ujuzi ambao utasaidia kuondoa umasikini,”alisema.

Akizungumza kuhusiana na misaada hiyo, mwanafunzi huyo amewataka wahisani wengine kuelekeza macho yao kwa watoto hao wenye ulemavu,kutokana na changamoto walizonazo ambazo baadhi yake wanaweza kushindwa kufikia ndoto zao.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa Elimu Jumuishi kitengo cha kanisa la FPCT wilaya ya Bahi na Dodoma, Jane Mgidange alisema serikali, taasisi, mashirika na watu binafsi wana jukumu kubwa la kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanatatuliwa changamoto zinazowakabili kwenye maisha yao.

“Mradi pamoja na kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu kuhusina na suala zima la kiafya na kielimu,pia tunaomba taasisi,mashika na watu binafsi kuhakikisha tunaisaidia serikali katika kuwaletea maendeleo kwa makundi maalumu katika kuinua uchumi wao,”alisema.

Alitaja vifaa vilivyotolewa ni pamoja ndoo za maji tiririka, sabuni ya kunawa mikono, vitakasa mikono, barakoa na vipeperushi ambavyo mbali na kutolewa shuleni pia wamevikabidhi kwenye familia wanazoishi watu wenye ulemavu.

JAMII imehadharishwa dhidi ya tabia ya ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine