loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kijana kortini kwa kudhalilisha kingono

JESHI la Polisi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora limemkamata Eva Timotheo Ernest (20) na kumpandisha kizimbani ajibu mashitaka ya kumfanyia vitendo vya ukatili wa kingono mtoto wa miaka miwili kwa kumuingizia kitu butu sehemu za siri.

Kijana huyo mkazi wa mtaa wa elimu kata ya Igunga amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Wilaya ya Igunga.

Mwendesha Mashitaka wa Polisi Wilaya ya Igunga Elimajid Kweyamba aliieleza Mahakama mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Igunga Lydia Ilunda kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu 38 C (1) (2) (b) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2019.

Majid alisema Julai 19 mwaka huu 2020 saa saba mchana katika eneo la Mtaa wa Elimu Kata ya Igunga mjini mshitakiwa alimfanyia ukatili wa kingono mtoto wa miaka miwili ambaye jina lake limehifadhiwa mwenye jinsi ya kike kwa kumuingizia kitu butu katika sehemu zake za siri na kumsababishia maumivu makali.

Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo, kesi imeahirishwa hadi Agosti 11 mwaka huu. 

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Igunga

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi