loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Samia: Msipojipanga tutawapanga kwa lazima

Makamu wa Rais, Samia Suluhu amewataka wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujitathmini katika michakato mbalimbali kama wamepita kwa sifa za weledi wao, au kwa rushwa.

Suluhu ameyasema hayo katika Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake CCM (UWT), maalum kwa ajili ya uchaguzi jijini Dodoma.

"Kiongozi mzuri ni yule anayepata uongozi kwa weledi bila rushwa, anayejiamini; sasa mjitathmini, mkishindwa kujipanga huku chini, basi juu tutalazimika kuwapanga," amesema.

Akaongeza: "Mzee wa mafaili (Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, Philip Mangula) ana tarifa ya kila mmoja, tutakapokutana maamuzi yoyote yatakayotolewa muwe ‘cool’ (mtulie) na mchape kazi," amesema.

Aidha, Mkamu wa Rais amezitaka jumuiya zote za chama hicho ikiwamo UWT kushikamana na kufanya kampeni za kweli ili kuiletea CCM ushindi wa kishindo kwa kuwa uchaguzi siyo kazi ndogo.

"Jukumu la kulainisha mchakato wa uchaguzi limeachwa kwa UWT hivyo mnatakiwa kujitoa hasa kwa kuwa jukumu lililopo mbele ni zito na siyo jepesi kama mnavyodhani,” amesema Mama Samia na kuongeza: "Kama mtu anaenda kwenye kampeni ajitoe hasa, siyo kujiendea tu na kufanya starehe, mjitoe kweli kweli."

Makamu wa Rais ametaka jumuiya hizo za CCM kujidhatiti na kuhakikisha ushindi unapatikana kwa pande zote mbili za Bara na Visiwani.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi