loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kalemani: Marufuku kuagiza vifaa nje, vijiji 2,800 kuwekwa umeme

SERIKALI imesema kuanzia Agosti 20, mwaka huu hadi Septemba 20, itaanza kusambaza wakandarasi kwenye vijiji na vitongoji mbalimbali  nchini kuunganisha umeme vijiji 2,800 vilivyobakia.

Pia, imesema haitaruhusu kuagizwa kwa kifaa chochote kutoka nje ya nchi kwa ajili ya utekelezaji  wa miradi ya nishati inayofanyika nchini.

Waziri wa Nishati,  Medard Kalemani amesema  hayo, Dar es Salaam   leo wakati akizindua kiwanda cha kuzalisha viunganishi vya umeme kutoka kwenye miundombinu mikubwa na kuusambaza  kwenda kwa wananchi  na wateja wengine kijulikanacho kama Inhemeter.

Alisisitiza matumizi ya vifaa vinavyozalishwa nchini katika miradi mbalimbali ya nishati.

Kuhusu matumizi ya vifaa ndani ya nchi, amesema hadi sasa serikali imefanya maboresho katika sekta hiyo ikiwemo kuweka zuio katika uagizwaji wa vifaa mbalimbali kutoka nje ya nchi, jambo ambalo limekuwa na manufaa makubwa.

Waziri Kalimani amesema  kuwa hadi sasa bidhaa za mita za umeme zinazalishwa nchini na kuna viwanda 13, viwanda vya kuzalisha nyaya vinne, transfoma viwanda vinne na  kwa sasa viunganishi vinapatikana nchini.

“Nilitoa miezi sita kuhakikisha vifaa hivyo vinapatikana nchini ambapo kwa sasa tunajivunia kuwa tayari kiwanda kimepatikana…hakuna haja ya kuagiza kifaa chochote kutoka nje ya nchi hususani kwa miradi inayotumia fedha za serikali,” amesema Kalemani. Aliongeza kuwa vifaa vyote vitakavyotumika vitatoka ndani ya nchi.

Kuhusu kuunganisha umeme kwenye vijiji, amesema  tayari  vijiji 9,512, kati ya 12,257 vilivyopo nchini, vimeunganishwa na nishati hiyo na vilivyobaki vitaanza kuunganishwa kuanzia Agosti 20, mwaka huu.

Amesema pia  miezi 11 imetengwa kwa ajili ya kufikisha umeme kwenye maeneo ambayo bado na serikali imetenga Sh bilioni 851 kwa ajili ya kukamilisha suala hilo.

Aliwaelekeza Wakala wa Umeme Vijijini (REA) na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuhakikisha wakandarasi watakaopewa kazi ya kufikisha umeme vijijini kutambua kuwa ni marufuku kuagiza vifaa nje yanchi.

Aidha aliwataka Tanesco kuagiza vifaa kwa viwanda vilivyopo nchini kwa ushindani wa bei. Alisitiza kiwanda hicho kuzingatia viwango bora vya uzalishaji, kutopandisha bei na kutofikiria kuuza nje ya nchi kwa sasa hadi  hapo taifa litakapojitosheleza.

Aliwapongeza kwa kuzalisha ajira 120 kwa watanzania  na alihimza wazalishaji na wajenzi wote nchini wa vifaa vya nishati kuonana na Tanesco kuonesha nia waliyo nayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Abraham Rajakili kwa upande wake amesema  kiwanda hicho kilianza kwa uzalishaji wa mita za luku za umeme nchini, na  kwa sasa kimeingia katika uzalishaji wa viunganishi hivyo wakiwa wamewekeza Sh bilioni tano.

Amesema wana uwezo wa kuzalisha viunganishi hivyo kwa aina tofauti  kwa uniti milioni 1.5 kwa mwaka ikiwa ni uzalishaji mkubwa. Wanatarajia kupanua soko kwa nchi nyingine kadri ya mahitaji.

Mwakilishi wa Mwekezaji wa kiwanda hicho, Mustafa Rashid yeye amesema “awali tulianza kuzalisha mita za luku na tulipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa serikali na zimekuwa zikitumika hapa hapa nchini na sasa tumeingia kwenye viunganishi,” 

JAMII imehadharishwa dhidi ya tabia ya ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

Habari Nyingine