loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tunajipanga upya- Lampard

KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema timu yake inajipanga upya baada ya kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa jumla ya mabao 7-1 na miamba ya Ujerumani Bayern Munich.

Mchezaji huyo wa zamani Chelsea mwenye rekodi ya kufunga, aliyefurahia maisha ya ushindi enzi zake kwa kushinda ubingwa wa Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa, amesema wanahitaji kujijenga upya ili kurejea mafanikio.

“Katika miaka 20 iliyopita tulikuwa na wachezaji kama (Eden) Hazard, (Diego) Costa, (Petr) Cech, (John) Terry na (Didier) Drogba,” alisema Lampard baada ya kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Bayern mwishoni mwa wiki iliyopita.

“Kutoa ushindani kwenye Ligi Kuu mwaka hadi mwaka na kucheza fainali na nusu fainali za michuano mikubwa sasa tunasuka mikakati ya kujipanga upya kurudia enzi za ushindi na mataji.”

Lampard aliyeiongoza Chelsea kumaliza ya nne kwenye Ligi Kuu na kucheza fainali za Kombe la FA katika msimu wake wa kwanza akiwa kocha, amesema katika msimu huu wa usajili anafanya utaratibu wa kukiimarisha kikosi chake.

“Tutatizama hilo, kwa sababu ni kazi yetu. Kutokana na kuwa kwenye kifungo cha kuzuiwa kusajili (mwaka jana) unaweza kuhisi yale tuliyoyakosa wakati wenzetu klabu nyingine waliyaoana,” alisema

LIVERPOOL inakaribia kumsajili kiungo ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine