loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Willian aaga Chelsea

WILLIAN ameandika katika mitandao yake ya kijamii kuwa anamaliza miaka yake saba ndani ya Chelsea msimu huu. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil amekuwa kwenye mazungumzo kuhusu mkataba mpya Stamford Bridge, lakini hawakufikia muafaka.

Vyanzo vinasema, mchezaji huyo mwenye umri wa maka 32 amekubali mkataba wa miaka mitatu Arsenal wenye mshahara wa karibu pauni 100,000 kwa wiki.

“Nilikuwa na miaka saba mizuri,” aliandika kwenye Twitter na kuongeza: “Agosti 2013 nilipopata ofa kutoka Chelsea, nilishawishika kuamini hii ndio klabu niliyotakiwa kucheza.”

“Leo nakiri kwamba ilikuwa maamuzi mazuri, kulikuwa na muda mwingi wa furaha, huzuni kidogo, kulikuwa na vikombe na mara zote ilifurahisha.”

“Mbali na vikombe, nimejifunza mengi kuhusu mimi mwenyewe kuwa mchezaji na mtu mwema, kwenye kila mazoezi, kwenye kila mechi, kila dakika niliyotumia kwenye chumba cha kubadilishia nguo mara zote nimejifunza.”

“Nimekuwa mwenye bahati kwa mashabiki wa Chelsea, walivyonikaribisha Stamford Bridge na sapoti yao kwa muda wote niliokuwa kwenye klabu yao.” “Kulikuwa pia na lawama, jambo ambalo ni kawaida...’’

LIVERPOOL inakaribia kumsajili kiungo ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine