loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Majaliwa afurahishwa na mfumo wa ‘T-Hakiki

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amefurahishwa na mfumo maalumu wa kuhakiki pembejeo za wakulima unaojulikana kama ‘T-Hakiki’ uliozinduliwa hivi karibuni na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), kuwasaidia wakulima kutambua ubora wa pembejeo kabla ya kuzitumia.

Waziri Mkuu amevutiwa na mfumo huo alipotembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya Wakulima,Wafugaji na Wavuvi maarufu Nanenane yaliyomalizika jana katika viwanja vya Nyakabindi Mkoa wa Simiyu.

Alisema mfumo huo ni mzuri endapo utatumika vizuri kwa wakulima na unaweza kuwasaidia kupambana na pembejeo feki. Akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba alisema mfumo huo umetokana na ubunifu wa TTCL, Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) na Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu Ukanda wa Tropiki (TPRI/TAPHPA), wakilenga kumsaidia mkulima kutambua pembejeo feki, ikiwemo dawa, mbegu na mbolea wanazotumia.

Kindamba alisema kuwa ubunifu huo umeenda sambamba na malengo ya Rais John Magufuli katika kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo. Kwa sasa huduma hii itamsaidia mkulima kufahamu matumizi sahihi ya pembejeo hizo kupitia simu ya mkononi.

Alisema kuwa T-Hakiki ni mfumo wa njia ya SMS Katika hatua nyingine, TTCL imeibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha watoa huduma za mawasiliano nchini na imechukua ushindi wa tatu wa jumla katika maonesho ya Nanenane kitaifa mwaka huu.

KAMPUNI ya uchimbaji ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Simiyu

Post your comments