loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Gharama za kupata wakili hazishikiki

KUPANDISHWA kwa ada ya mawakili, kumesababisha ugumu kwa wananchi kupata huduma ya mawakili kutokana na wengi kutomudu kiwango kikubwa cha malipo kinachotakiwa.

Baraza la Mawakili nchini Uganda limefanya uamuzi wa kupitia upya viwango vya ada na kuamua kupandisha ili kuendana na gharama za maisha ambazo zimepanda.

Baraza hilo ni chombo cha serikali chenye mamlaka ya kushughulikia masuala ya taaluma ya sheria na utoaji wa misaada ya kisheria nchini humo.

Kwa mujibu wa viwango vipya vya mishahara na kodi vilivyopitishwa, ambavyo vimefanyiwa mabadiliko kwa kutumia Sheria ya mwaka 2020, wakili mmoja atalipa katika kesi ya uchaguzi ya ubunge kiasi kisichopungua Sh milioni 10 za Uganda.

Kipengele hicho kilichopitishwa na Mwenyekiti wa Baraza la Sheria, Jaji Remmy Kasule kinasema mwanasheria anatakiwa kulipa si chini ya Sh milioni tano kwa ajili ya kumwakilisha mteja katika kesi ya uchaguzi wa serikali za mtaa.

Kutokana na viwango hivyo, wananchi wanapata shida ya kupata huduma ya uwakili kutokana na kutakiwa kulipa fedha nying,i baada ya ada wanayolipa mawakili kupandishwa.

Waliotengeneza na kupitisha Sheria hiyo ya mwaka 2020, wanasema kuwa kuna mambo kadhaa yaliangaliwa na kuzingatiwa, kabla ya kupitisha ada mpya ya wanasheria.

Walitaja baadhi ya mambo hayo kuwa ni mazingira, umuhimu, ugumu, mahali na hali halisi ambapo kazi hiyo inafanyika, muda unaotumika na maslahi ya umma.

foto
Mwandishi: KAMPALA

Post your comments