loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wafuasi wa Bobi Wine wapambana na polisi

POLISI katika mji wa Mbale wamefanikiwa kuwatawanya wafuasi wa chama cha National Unity Platform (NUP) kinachoongozwa na mwanamuziki, Roberty Kyagulanyi maarufu Bobi Wine (pichani), walipofanya maandamano yasiyo halali.

Mwanasiasa huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyandondo Mashariki, alipanga kufika katika mkutano wa hadhara, uliotarajiwa kufanyika kuanzia saa 3:00 hadi 5:00 asubuhi kuzungumza na wananchi.

Lakini polisi waliupiga marufuku mkutano huo, kwa sababu haukuwa halali kutokana na waandaaji kutofuata masharti na vigezo vinavyohitajika ili kibali kiweze kutolewa.

Kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya polisi kutangaza mkutano huo ni batili na watu wote waliokuwepo katika mkusanyiko huo kutakiwa kutawanyika, wafuasi wa chama hicho hawakutii amri hiyo.

foto
Mwandishi: MBALE

Post your comments

Habari Nyingine