loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mboga, mkaa vyaongeza mfumuko wa bei

KUPANDA kwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa asilimia 0.1 kutoka asilimia 3.2 hadi 3.3, kumechangiwa na kupanda kwa bei ya mboga kwa asilimia 9.6 na mkaa kwa asilimia 11.6.

Mfumuko uliopanda ni kwa mwaka unaoishia Julai mwaka huu kutoka mwaka ulioishia Juni mwaka huu. 

Akizungumza jana jijini Dodoma, Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu,(NBS), Ruth Minjaalisema ukiachia mbali mboga, bidhaa nyingine za chakula zilizochangia kupandisha mfumuko wa bei ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia 7.9, mtama 4.8%, unga wa muhogo 3.0%, dagaa asilimia 3.8 na matunda 4.0%.

Ruthi alisema bidhaa nyingine zisizo za vyakula zilizapandisha mfumuko wa bei ni pamoja na mavazi kwa asilimia 2.8, gesi ya kupikia kwa asilimia 5.9, samani kwa asilimia 2.7 na gharama za utengenezaji na ukarabati nyumba 6.2%. 

Alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa Julai mwaka huu umebaki 3.8% kama ilivyokuwa kwa mwaka unaoishi Juni, mwaka huu.

Katika nchi za Afrika Mashariki (EAC), nchini Kenya mfumuko wa bei umepungua kutoka asilimia 4.59 hadi 4.36%.

Nchini Uganda, mfumuko wa bei wa taifa hilo umeongezeka hadi asilimia 4.7 kutoka asilimia 4.1 kwa mwaka unaoishi Juni, mwaka huu.

Mfumuko wa bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya nchini.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ndiyo yenye jukumu la kutoa, kusimamia na kuratibu upatikanaji na usambazajio wa takwimu rasmi nchini ikiwa ni pamoja na takwimu za mfumuko wa bei kwa ajili ya matumizi ya serikali na wadau.

TIMU ya  Simba imethibitisha kiungo  wake Mbrazili Gerson Fraga ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi