loader
Dstv Habarileo Mobile
Picha

Simba yamuwekea kizuizi Senzo Yanga

SIKU moja baada ya aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba,  Senzo Mazingiza, kuacha kazi katika klabu hiyo na kuhamia Yanga SC, amepewa masharti na waajiri wake hao wa awali ya kuyafuata ili aendelee na kazi zake vizuri hapa nchini.

Senzo raia wa Afrika Kusini anaaminika kuwa ni kiungo muhimu katika kukamilisha usajili wa mchezaji yoyote, ambaye klabu itamuhitaji.

Akizungumzia sakata la kuondoka kwa Senzo, Mshauri wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Cresentus Magori, jana alidai kitendo alichokifanya Senzo sio kizuri na hakikuwafurahisha.

Alisema wamepokea kwa mshituko taarifa zake za kuacha kazi, lakini anapaswa ajue kuwa hawezi kufanya kazi Yanga kama hataomba idhini ya Simba.

Alisema Simba ndio walimuombea kibali cha kufanya kazi nchini, hivyo hawezi kufanya kazi kwingine kama mabosi wake wa zamani hawajatoa ruhusa.

"Alipaswa kutoa taarifa rasmi ndipo aache kazi kwakuwa kuna vitu ambavyo anatakiwa akabidhi ikiwamo ofisi, sasa kaondoka na hapatikani kwenye simu sio jambo zuri.”

"Wakati anakuja hapa nchini sisi ndio tulimuombea kibali cha kufanya kazi baada ya kutoa maelekezo kuwa apewe kibali hicho, hivyo kama Yanga wanataka awafanyie kazi wanatakiwa waje kwetu kupata kibali," alisema Magori.

foto
Mwandishi: Mohammed Mdose

5 Comments

 • avatar
  Chizi mpira
  11/08/2020

  Nyie mkia nafanya kazi za Uhamiaji!?

 • avatar
  Chizi mpira
  11/08/2020

  Nyie mkia nafanya kazi za Uhamiaji!?

 • avatar
  Deo
  11/08/2020

  Kwani Simba SC ndio Uhamiaji? Sisi Yanga tutaomba kibali upya, kaombeni chenu wakifute.

 • avatar
  Ayubu
  12/08/2020

  Kibali tutamuombea kipya. Nyie Cha kwenu mfutie kabisa, tutaomba kipya

 • avatar
  Josia Luhunga
  12/08/2020

  Amakweli mumekua uhamiaji sasa mtapatatabu sanaaaa

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi