loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waonywa kujihusisha na itikadi Uchaguzi Mkuu

WASIMAMIZI wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya kata katika jimbo la Mbinga Mjini mkoani Ruvuma wameonywa kujiepusha kufanya kazi kwa itikadi za vyama vya siasa na kupendelea wagombea.

Badala yake watende haki kwa kila chama wakati wote wa mchakato wa uchaguzi ili kuepusha vurugu na malalamiko.

Rai hiyo ilitolewa jana na Ofisa uchaguzi jimbo la Mbinga, Amon Sangana wakati akifunga mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wasimamizi wasaidizi 38 wa uchaguzi ngazi ya kata na jimbo, mafunzo yanayolenga kuwaongoza katika mchakato mzima wa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Oktoba.

Aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kwenda kutekeleza vema yale waliofundishwa ikiwemo suala la uadilifu, weledi na kujiepusha na aina yoyote ya upendeleo kwa vyama vya siasa na wagombea.

Kwa upande wake Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mbinga Mjini, Grace Quintine alisema matumaini ya Tume ya Uchaguzi kwamba baada ya kupata mafunzo hayo watakwenda kufanya kazi kwa juhudi, maarifa na weledi wa hali ya juu.

Quitine ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mbinga alisema, wakati wote wa miezi mitatu ya mchakato wa uchaguzi mkuu watafanya kazi kwa kufuata maelekezo ya tume na msimamizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na kushirikiana na vyama vyote vya siasa vitkavyoshiriki katika uchaguzi huo.

Aidha alisisitiza suala zima la kuzingatia maadili ya utumishi wa umma wakati wa mchakato wa uchaguzi pamoja na kufanya kazi nyingine za utumishi ikiwemo kuuza vitambulisho vya wajasiriamali vilivyotolewa na Rais John Magufuli.

JAMII imehadharishwa dhidi ya tabia ya ...

foto
Mwandishi: Muhidin Amri, Mbinga

Post your comments

Habari Nyingine