loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Minael-Hossana: Kifo cha Mkapa kimenikumbusha wema wa Nyerere

BABA wa Taifa, Mwalimu Julius K Nyerere, ndiye Rais wa Kwanza wa Tanzania. Alifariki dunia Oktoba 14, 1999. Wakati huo, Benjaim William Mkapa ndiye alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya Tatu baada ya Nyerere kumpigia debe Mkapa katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 1995 uliokuwa wa kwanza katika mfumo wa siasa wa vyama vingi uliorejea nchini mwaka 1992.

Mkapa amefariki Julai 24, 2020. Minael- Hossana Mdundo, anasema katika maisha yake, hatasahau mchango wa wanasiasa hao waliokuwa wakuu wa nchi.

Huyu, ni mwanamke aliyestaafu utumishi wa umma katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mwaka 2013 baada ya kulitumikia tangu mwaka 1982.

Alistaafu akiwa katika cheo cha Meja. Ndiye mwandishi wa kitabu cha ‘Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha’ cha mwaka 1999 ambacho utangulizi wake, umeandikwa na Marehemu Mwalimu Julius K. Nyerere baada ya kuombwa na Thabiti Kombo kikiwa kimehaririwa na Paul A. Sozigwa.

Anasema uzinduzi wa kitabu hicho Julai 19, 2000 ulifanywa na Rais wa Zanzibar wakati huo, Dk Salmin Amour, uihudhuiriwa na Makamu wa Rais, Dk Omar Ali Juma visiwani Zanzibar kwa sababu masimulizi yake yanahusu Zanzibar.

Sherehe ziliandaliwa kwa udhamini wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere. Hossana anasema kifo cha Mkapa kilichotokea mwezi uliopota jijini Dar es Salaam, kimemtia simanzi na kumbusha fadhila walizomfanyia pamoja na Mwalimu Nyerere kabla hajafariki dunia.

 

 

 

 

 

Anasema anawakumbuka kwa mchango mkubwa uliotolewa na Nyerere ikiwa ni pamoja na msaada ukiwamo wa kuandika utangulizi wa kitabu chake, huku Mkapa akiwa Rais wakati huo, akifanikisha kupata Sh 1,000,000, ziizokuwa zimetolewa na Mzee li Hassan Mwinyi; Rais wa Awamu ya Pili kabla hajastaafu. Katika sehemu za utangulizi wa kitabu hicho chenye kurasa 270, Mwalimu Nyerere anaandika: “Tarehe 5, Februari 1957, nilikwenda Zanzibar kwa bahati tu. Nilikuwa na mgeni wangu wa kutoka Marekani aliyetaka sana kufika Zanzibar. Tukafuatana siku hiyo.: “Na kumbe siku yenyewe, ndiyo vyama vya African Association na Shirazi Association vilikuwa vimepanga kuzungumzia ushirikiano wao katika harakati za ukombozi; bila shaka kwa maelewano na wenzake wa Shirazi Association, alinikaribisha katika mkutano huo wa kihistoria.” Nyerere anasema: “Nilikuwa siwafahamu vizuri viongozi wa Shirazi Party. Lakini katika mkutano huo, Sheikh Thabiti Kombo, Katibu Mkuu wa chama hicho, alidhihirika kuwa mtu hodari sana. Ndiye aliyependekeza na kutoa hoja za kuunganisha vyama hivyo. Na ndiye aliyependekeza Karume awe kiongopzi wa chama hicho kipya. Karume naamini kwa moyo na nia safi kabisa, hakutaka kuwa kiongozi wa chama kipya hicho.” “Lakini ni Sheikh Thabiti Kombo aliyeng’ang’ania kabisa Karume awe kiongozi wa chama kipya hicho. Bila busara, hekima na ujasiri wa Sheikh Thabiti, pengine vyama hivyo visingeungana au kama vingeungana, baadaye ungetokea mzozo mkubwa kuhusu uongozi na historia nzima ya ukombozi wa Zanzibar na kwa hiyo, historia ya Tanzania ingekuwa tofauti.” Nyerere anasema: “… Kabla ya kufariki, Sheikh Thabiti alipata wazo la kusimulia katika kanda visa mbalimbalimbali vilivyompata yeye mwenyewe na kwa namna yake. Ameyasema akiwa mtu mzima sana na kutokana na kumbukmbu zake tu.” “Lakini Sheikh habit alikuwa ni mtu mwenye kumbukumbu nzuri sana; na alitaka vizazi vyote vya Watanzania viyajue hayo aliyosimulia, na kwa kuelewa hivyo wapate kutambua chimbuko la umoja wa taifa letu na faida za umoja huo.” Katika Kitabu hicho Nyerere anasema: “Kazi ya kuhariri masimulizi ya Sheikh Thabiti ili yaandikwe katika kitabu hicho imefanywa na Kapteni (wakati huo) Minael Mdundo na Paulo Sozigwa. Wote wawili napenda kuwapongeza kwa kazi nzuri waliyoifanya. Lakini Kapteni Minael Mndundo anastahili sifa za kipekee.” “Ndiye aliyekaa muda mrefu pamoja na Sheikh Thabiti na kumsikiliza na kuyatia masimulizi yake katika kanda. Na kwa heshima aliyokuwa nayo kwa Mzee Thabiti, binti huyo amefanya utafiti mzuri sana kuhusu historia ya African Association na harakati za awali za ukombozi wa sehemu hii ya Afrika. Na kazi hii ameifanya kwa uvumilivu mkubwa sana. Labda kwa sasa Kapteni Minaeli Mdundo anajua historia ya African Association vizuri zaidi kuliko mtu mwingine yeyote aliye hai hivi sasa. Nampongeza sana.” Mada zilizo katika kitabu hicho cha ‘Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha’ ni Asili ya Watu wa Zanzibar; Maisha Yake; Ukoo Wake na Kazi Zake; Kutumbukia kwa Waingereza; Maisha ya Siasa ya Wananchi wa Zanzibar; Uchaguzi wa Kwanza; Uchaguzi wa Pili, Januari 1961 na Uchaguzi wa Tatu, Juni 1961. Nyingine ni Misukosuko ya Mwisho na Mikutano ya Kikatiba; Mapinduzi ya Afro-Shirazi Party Januari, 1964; Wasaliti wa Mapinduzi ya Afro Shirazi Party; Kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi; Mabadiliko ya Katiba na Mabadiliko ya Uongoz wa Juu. Mwandishi huyu anasema kifo cha Mkapa kimemkumbusha namna alivyomsaidia kwa kukubali kuhuisha hundi ya Sh milioni moja aliyokuwa amepewa na Mzee Mwinyi akiwa rais, lakini ikaisha muda wake kabla hajachukua fedha hizo kwa ajili ya maandalizi ya awali ya kitabu hicho. “Kifo cha Mkapa kimenikumbusha sana na kunifanya niendelee kumshukuru kwa kukubali kuhuisha hundi iliyokuwa imechacha tayari na pia, ninamshukuru sana Mkapa kwani katika hotuba yake katika Maadhimisho ya Miaka 40 ya Muungano Aprili 26, 2004 akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alinitaja katika Uk wa 9 wa hotuba yake; mimi, mhariri na kampuni iliyochapa kitabu changu.” Katika maadhimisho hayo, Mkapa alisema: “…Historia halisi ya Kiafrika kwa kiwango kikubwa ni historia simulizi. Na ingawa ametangulia mbele ya haki, napenda xx Minael-Hossana: Kifo cha Mkapa kimenikumbusha wema wa Nyerere Mwandishi wa Kitabu cha ‘Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha’ , Minael-Hosanna O. Mdundo (kulia) akikabidhi nakala ya kitabu hicho kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta (sasa ni marehemu) jijini Dodoma April 24, 2014. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba (Sasa ni Makamu wa Rais) Samia Suluhu Hassan. Na Joseph Sabinus BABA wa Taifa, Mwalimu Julius K Nyerere, ndiye Rais wa Kwanza wa Tanzania. Alifariki dunia Oktoba 14, 1999. Wakati huo, Benjaim William Mkapa andiye alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya Tatu baada ya Nyerere kumpigia debe Mkapa katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 1995 uliokuwa wa kwanza katika mfumo wa siasa wa vyama vingi uliorejea nchini mwaka 1992. Mkapa amefariki Julai 24, 2020. Minael- Hossana Mdundo, anasema katika maisha yake, hatasahau mchango wa wanasiasa hao waliokuwa wakuu wa nchi. Huyu, ni mwanamke aliyestaafu utumishi wa umma katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mwaka 2013 baada ya kulitumikia tangu mwaka 1982. Alistaafu akiwa katika cheo cha Meja. Ndiye mwandishi wa kitabu cha ‘Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha’ cha mwaka 1999 ambacho utangulizi wake, umeandikwa na Marehemu Mwalimu Julius K. Nyerere baada ya kuombwa na Thabiti Kombo kikiwa kimehaririwa na Paul A. Sozigwa. Anasema uzinduzi wa kitabu hicho Julai 19, 2000 ulifanywa na Rais wa Zanzibar wakati huo, Dk Salmin Amour, uihudhuiriwa na Makamu wa Rais, Dk Omar Ali Juma visiwani Zanzibar kwa sababu masimulizi yake yanahusu Zanzibar. Sherehe ziliandaliwa kwa udhamini wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere. Hossana anasema kifo cha Mkapa kilichotokea mwezi uliopota jijini Dar es Salaam, kimemtia simanzi na kumbusha fadhila walizomfanyia pamoja na Mwalimu Nyerere kabla hajafariki dunia. Anasema anawakumbuka kwa mchango mkubwa uliotolewa na Nyerere ikiwa ni pamoja na msaada ukiwamo wa kuandika utangulizi wa kitabu chake, huku Mkapa akiwa Rais wakati huo, akifanikisha kupata Sh 1,000,000, ziizokuwa zimetolewa na Mzee li Hassan Mwinyi; Rais wa Awamu ya Pili kabla hajastaafu. Katika sehemu za utangulizi wa kitabu hicho chenye kurasa 270, Mwalimu Nyerere anaandika: “Tarehe 5, Februari 1957, nilikwenda Zanzibar kwa bahati tu. Nilikuwa na mgeni wangu wa kutoka Marekani aliyetaka sana kufika Zanzibar. Tukafuatana MAKALA kumshukuru sana Marehemu Thabiti Kombo Jecha ambaye ameachia vizazi vinavyomfuata masimulizi ya maisha yake, masimulizi ambayo ni hazina kubwa kwa watafiti na kwa yeyote mwenye nia ya kujua historia ya Zanzibar, historia ya Tanzanua na historia ya Bara la Afrika.” “Masimulizi hayo yameandikwa na Kapteni Minael-Hossana Mdundo na kuhaririwa na Ndugu Paul Sozigwa, na kuchapwa na kampuni ya Uchapishaji ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam…” Minael-Hossana Mdundo anasema: “Namshukuru sana Mkapa kwani licha ya kuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati huo, mimi nikiwa na cheo kidogo tu cha Meja wa JWTZ ingawa katika kipindi cha mwalimu nilikuwa kapteni, alionesha unyenyekevu na utaalamu katika taaluma baada ya kutumia kazi yangu na kunitaja. Kwa kweli ninamshukuru sana.” Anasema siku hiyo alikuwa chumbani kwake akifuatilia hotuba na ndipo alipomsikia Rais Mkapa (wakati huo) akitaja jina lake na jina la kitabu chake na hapo hapo akaanza kupokea simu kutoka kwa watu mbalimbali wakiwamo wafanya kazi na wakubwa zawe wakimpongeza. “Hata nilipoingia bwaloni, japo nilikuwa na cheo kidogo, maofisa walinipongeza na kunishangilia kwa furaha… Kwa kweli nilipanga na kwenda kanisa kumshukuru Mungu kwa mtu mdogo kama mimi kazi yangu kuonwa na kutumiwa na Mkuu wa Nchi…. Japo hakuwahi kuniita, lakini siku hiyo niliona ni tukio la kushitukiza, lakini la furaha kubwa kwangu.” Kwa mujibu wa Hossana, anasema anamshukuru Mkapa kwa sababu: “Alipotumia jina na kitabu changu katika hotuba yake, jina langu lililokuwa katika utaratibu wa kusubiri, lilipitishwa na mimi kwenda masomoni.” “Alitumia jina langu wiki hii, wiki ijayo Kanali Juma Ikangaa akakitumia kushawishi hivyo utaona kutumia kwake kazi yangu, kulinisaidia kupewa ruhusa haraka kwenda kusoma katika Chuo cha Ukutubi na Utunzaji Nyaraka (School of Librarianship Archives and Documentation) maana nilikuwa katika orodha ya kungoja, lakini kazi yangu imeonekana hadi kwa Amiri Jeshi Mkuu; nikapewa nafasi haraka…” Anasema katika chuo hicho, alisoma Stashahada ya Nyaraka (Archives) kwa miaka miwili. Nilikuwa tayari Meja, lakini baadaye, nikaingia katika mambo ya ‘peace keeping’ (ulinzi wa amani). Mwandishi huyo wa ‘Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha’ anasema Watanzania wawakumbuke na kuwaenzi Nyerere na Mkapa kwa kuendeleza moyo wa shukrani na kuimarisha mema waliyoyatenda viongozi hao wakubwa wa kisiasa nchini na wenye sura na sifa bora zisizofutika kimataifa. Alipoulizwa sasa anafanya nini kuwaenzi zaidi viongozi hao maarufu duniani, Minael Mdundo anasema: “Hata sasa kuna mambo ya Mwalimu Nyerere ninayofuatilia ambayo kwa sasa sipendi yaandikwe.” “Aidha, ninashughulikia hadidu za rejea teule kuhusu umajumui wa Afrika uliotokana na Nyerere ukitekelezwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Mkapa tangu akiwa Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu na hata alipokuwa Rais wa Awamu ya Tatu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania…. “

WAKATI Rais John Magufuli ...

foto
Mwandishi: Joseph Sabinus

Post your comments

Habari Nyingine