loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

ACT- Wazalendo yataka wagombea kuwa makini

CHAMA cha ACT- Wazalendo kimewataka wagombea nafasi ya ubunge na udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba wasirubuniwe na wapinzani wao, badala yake wasimame na kutetea nafasi hizo mpaka hatua ya mwisho.

Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Kabwe Zitto aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa chama hicho mjini hapa.

Alisema imekuwa tabia wanachama wanapatiwa nafasi ya kugombea udiwani na ubunge baada ya muda wanaambiwa alitoroshwa kumbe alirubuniwa na mpinzani wake.

Alisema kuwa, “unapoweza kuaminiwa na wanachama wenzako ugombee nafasi hizo, basi nawe ujiaminishe kwao kupigania mpaka hatua za mwisho wa uchaguzi, siyo kukubali kwa haraka haraka, huo ni usaliti kwa wenzako”.

Alisema katika ngazi ya udiwani kwa jimbo la Lindi Mjini kwenye kata 20 zinawezekana kuchukuliwa na chama hicho na pia viti maalumu vya udiwani vikaongezeka kutokana jinsi idadi ya madiwani wa kata watakavyoshinda.

Katika mkutano huo uliofanyika mjini hapa, ACT iliweza kumpitisha Mwenyekiti wa chama hicho mkoa, Isihaka Mchinjita kuwa mgombea ubunge wa jimbo la Lindi Mjini.

Mchinjita aliwataka wanachama kuwa kituo kimoja wakati huu wa uchaguzi.

Aidha pia kiliweza kutoa mapendekezo kwa kuwapitisha wagombea wa viti maalumu udiwani, akiwemo Mwajuma Mtenda aliyepata kura 143 akifuatiwa Hawa Kipara aliyepata kura 132 katika kinyang’anyiro hicho.A

RAIS John Magufuli ameagiza ...

foto
Mwandishi: Kennedy Kisula, Lindi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi