loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bodi ya Mfuko wa Barabara yapewa wiki daraja Kiegeya

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe ameipa wiki moja Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini kutoa Sh bilioni nne kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Kiegeya barabara kuu ya Morogoro- Dodoma ambalo Machi 2, mwaka huu lilibomolewa na mafuriko ya maji ya mvua.

Kamwelwe alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea eneo la Kiegeya na kukagua hatua za mwisho ya maandalizi ya kuwekwa lami baada ya kujengwa kwa barabara ya mchepuo na maandalizi ya ujenzi wa daraja la mwanzo.

“Tumekamilisha maandalizi yote ya kujenga daraja la kudumu eneo lilipovunjika kwa mafuriko ya maji ya mvua na tarataibu za manunuzi zimekamilika,” alisema na aliongeza:

“Daraja hili litajengwa kwa direct labour ambao ni Tanroads (Wakala wa Barabara Tanzania) wenyewe wataleta wataalamu na kwa sababu taratibu zimefanyika naaiagiza Tanroads kazi hii ianze jumatatu wiki ijayo”.

Alisema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo Desemba mwaka huu, barabara hiyo itakuwa imekamilika na magari mengine yatamahishiwa kupita juu na barabara hiyo kama ilivyokuwa hapo mwanzo.

“ Ninayo taarifa ya kwamba Tanroads imeandika barua ya kuomba fedha , sasa naiagiza Bodi ya Mfuko wa Barabara kama hawajaweka fungu la fedha za kujenga daraja hili halikuwepo, bodi toeni Sh bilioni nne katika muda wa wiki moja na ziwe zimeletwa Tanroands Morogoro kwa ajili ya kujenga daraja hili,”alisema.

Waziri Kamwelwe alisema kiasi hicho kinatokana na makadirio yaliyofanyika na wataalamu wa ujenzi wa daraja hilo na ndicho kinachotarajiwa kukamilisha ujenzi wa daraja la Kiegeya.

Kuhusu barabara ya mchepuo inayotumika kwa hivi sasa, alisema imejegwa na kuwekewa matabaka mawili ya udongo uliochanganywa na saruji na hivyo kuwa na unene wa sentimeta 40.

Alisema kazi iliyopo ni uwekaji lami ambayo inatarajia kuanza Augosti 14, mwaka huu na hivyo kuifanya barabara hiyo kuwa ni ya kudumu .

“Barabara ya mchepuo itaendelea kuwepo na itasaidia kwenye dharura na sehemu ya zamani daraja litakapojengwa na kukamilishwa na magari mengine yataendelea kupita eneo hilo,” alisema.

Naye Meneja wa Tanroads mkoa, Nkolante Ntije alisema watasimamia kazi hiyo kwa nguvu zote ili ikamilike kwa muda uliopangwa kwa kuwa vifaa vyote vipo na vingine vitaletwa na wakandarasi wenyewe.

Pia alisema tayari wamewasiliana na Tanesco ili kuwekewa Transfoma kwenye njia yao ya umeme uliyopita katika eneo hilo kwa ajili ya mitambo ambayo haitakuwa na uwezo wa kutumia umeme wa jenereta.

VIJIJI 73 kati ya vijiji 77 vya Wilaya ya Missenyi ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi