loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kataa Kudhalilishwa, NEC Chukueni Hatua

TUME YA Taifa ya Uchaguzi (NEC), na vyombo vya dola nchini, vimetakiwa kuchukua hatua kali  dhidi ya wanasiasa na watu wanaotoa lugha za udhalilishaji kwa wanawake.

Hayo yamesemwa  na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa), Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) pamoja na Global Peace Foundation (GPF) katika tamko lao kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliopangwa kufanyika Oktoba 28.

Akisoma tamko hilo leo Jumatano  Agosti 12, Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa, Rose Reuben amesema asasi hizo ziliendesha midahalo hivi karibuni kutoka vyama vya siasa, viongozi wa dini, wanawake wanasiasa na waandishi wa habari chini ya ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake Afrika (AWDF) kupitia  mradi wa ‘Wanawake Sasa’.

Mkurugenzi huyo wa Tamwa amesema kupitia midahalo mbali mbali ambayo waliendesha wamebaini changamto  zinazosababisha ushiriki mdogo wa wanawake katika siasa na kuvitaka vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi, kuondoa changamoto hizo.

“Tumebaini uwepo wa vitendo vya kuombwa au kutengenezewa mazingira ya rushwa ya ngono na  baadhi ya wanaume wenye dhamana ya kusimamaia michakato ya chaguzi au mamlaka za ndani ya vyama vya siasa,” amesema

 Reuben amesema kuwa changamoto hizo zinavunja moyo wanawake wengi hivyo kutoshiriki shuguli za kisiasa au kukosa nafasi za uongozi pale wanapokuwa na msimamo wa kutotoa rushwa.

“Katika hili tunatoa rai kwa wanawake wenzetu, kukataa kabisa kudhalilishwa na kutojihusisha na vitendo vya rushwa ya fedha au ngono….; “Tunatoa rai pia kwa jumuiya za wanawake ndani ya vyama vya siasa kuvunja ukimya na kuhakikisha hoja za rushwa katika siasa inazungumzwa kwa sauti kubwa katika kila vikao vya jumuiya na vikao vingine muhimu.

Aidha pia  wamevitaka vyama vya siasa kuweka utaratibu wa siri wa kutoa taarifa za vitendo hivyo na kuwe na kamati huru ndani ya vyama  zisizofungamana na yeyote zitakazoratibu upokeaji, ufuatiliaji na utoaji wa adhabu kwa wale ambao bado wanaendekeza vitendo hivyyo vya kudhalilisha wanawake.

Kuhusu ushiriki wa wanawake, Rose alisema muitikio wa wanawake katika uchaguzi wa mwaka huu unatia moyo kwani kati ya kati ya wagombea 16 waliochukua fomu kugombea urais, wapo wanawake wawili mpaka sasa ambao ni Queen Cathbert Sendinga wa Chama cha ADC, na Cecilia Augustino wa Demokrasia Makini walioteuliwa na vyama vyao kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi huo.

 Kadhalika, wapo wanawake watano wanaowania umakamu wa Rais, katika mchakato huu wa uchaguzi.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi