loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Chadema, NDC na AAF wafungua pazia ubunge Dar

Wagombea kutoka vyama vya upinzaji vya Chadema, NDC na AAFP wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania ubunge katika majimbo matatu ya Dar es Salaam.

Mgombea wa AAFP, Ndonge Said Ndonge amebainisha kuwa anawania jimbo la Mbagala kutokana na kuguswa na changamoto kadhaa zinazolikabili jimbo hilo na kuwa akipewa ridhaa ya wananchi ya kuliongoza atazitatua na kuwainua zaidi kimaisha.

Amesema,”Hakika wakazi wa Mbagala hawatajuta kunichagua kuwania nafasi hii, nimejipanga na nipo vema zaidi kuwaongoza kwa kila hali, jimbo litakuwa na maendeleo na leo nimechukua fomu kuanza safari ya kuwaendeleza.”

Naye Msimamizi wa uchaguzi wa majimbo ya Temeke na Mbagala, Lusubilo Mwakabibi, amebainisha kuwa hadi kufikia  mchana wa leo  ni mgombea mmoja tu  aliyekuwa amejitokeza.

Kwa upande wa Ilala yenye majimbo ya uchaguzi ya Ukonga, Segerea na Ilala yenyewe, Msimamizi wa uchaguzi, Jumanne Shauri amebainisha wagombea wawili wamejitokeza  kuwania ubunge ambao ni Carlen Mkumbo wa chama cha ADC anayewania Ukonga na John Mrema anayewania Jimbo la Segerea kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema).

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi