loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ajuza aomba JPM amsaidie kupata eneo alilouza mwanawe

MKAZI wa Kijiji cha Nkoaranga, wilayani Arumeru mkoani Arusha, Ndesinio Ndewario (94) amemuomba Rais John Magufuli amsaidie kupata eneo lake baada ya kushinda kesi mahakamani.

Ndesinio aliwaeleza waandishi wa habari jijini Arusha kuwa, alishitakiana na mtoto wake aitwaye Emmanuel Nko anayedaiwa kuuza eneo hilo lenye ukubwa wa ekari moja Kiwawa wilayani humo.

Alidai kuwa, katika kesi mbalimbali kuanzia Baraza la Ardhi la Kata, Baraza la Ardhi la Wilaya, Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa alishinda na kwamba mahakama hizo zilimtambua kuwa yeye ni mmiliki halali wa eneo hilo.

Ajuza huyo alidai kuwa, mwanawe huyo aliuza eneo kinyemela kwa Ester Palangyo mwaka 2012.

Alidai kuwa, Ester ni mkazi wa Maji ya Chai wilayani Arumeru na kwamba Emmanuel aliuza eneo bila kuishirikisha familia wakati akifahamu kuwa si mali yake na ni kinyume cha sheria.

Ndesinio alidai kuwa baada ya kumalizika kesi Mahakama Kuu, Mahakama ya Rufaa ilitoa maelekezo kuwa kesi hiyo irejeshwe Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Arumeru ili litekeleze amri ya mahakama hiyo kwa kukabidhi eneo kwa mdai.

Baraza hilo la Ardhi na Nyumba la Wilaya lilimwandikia barua Mkuu wa Wilaya ya Arumeru yenye kumbukumbu namba DLHT/MISC.APP.NO.48 ya mwaka 2013 kuitambulisha kampuni ya udalali ya Regiz Companya Ltd kwa ajili ya utekelezaji wa amri ya baraza katika shauri namba 48/2013 ya mdai Ndesinio Ndewario dhidi ya mdaiwa Emmanuel Ndewario Nko.

Alidai kuwa Kampuni ya udalali ya Regiz kupitia barua yenye kumbukumbu namba RGZ/AR/48/2020 ilitekeleza hukumu ya shauri hilo namba 48/2013, ikiwa ni pamoja na kuondoa nyumba zilizokuwa zimejengwa na kumkabidhi mdai mbele ya watendaji wa ofisi ya kata ya Imbaseni wilayani humo.

Ndesinio alidai kuwa, Julai 23 mwaka huu alipokea barua kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro yenye kumbukumbu namba DC/ ARUM/W.10/1XL/62 ya kusitisha kufika katika eneo hilo, jambo ambalo amedai ni ukiukwaji wa amri ya Mahakama.

Amemuomba Rais Magufuli aingilie kati kumsaidia kupata eneo lake kwa madai kuwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya haina uwezo wa kupinga amri ya mahakama. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro alikiri kuandika barua hiyo baada ya kubaini kuwepo kwa viashiria ya uvunjifu wa amani

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi