loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

ZEC yafafanua upigaji kura siku moja kabla

MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jaji mstaafu Hamid Mahmoud amesema kura ya mapema ipo kwa mujibu wa sheria na itafanyika kwa ajili ya kuwapa nafasi wafanyakazi na wasimamizi wa uchaguzi pamoja na watendaji wa vyombo vya ulinzi kutekeleza haki yao kidemokrasia kuchagua viongozi.

Jaji mstaafu Mahmoud alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mafunzo ya siku moja kuhusu sheria za uchaguzi na majukumu ya ZEC kwa mujibu wa sheria.

Alisema Sheria ya Uchaguzi kifungu cha 82 cha sheria hiyo nambari 4 ya mwaka 2018 imetoa nafasi kwa wasimamizi wa uchaguzi, wasaidizi wasimamizi wa uchaguzi pamoja na vyombo vya ulinzi watakaofanya kazi katika kipindi cha uchaguzi kushiriki katika uchaguzi huo.

“Napenda kuwajulisha wananchi kwamba kura ya mapema ipo kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi nambari 4 ya mwaka 2018 na upigaji kura utawahusisha wasimamizi wa uchaguzi pamoja na watendaji wa Tume na wafanyakazi wa vyombo vya ulinzi watakaokuwepo katika siku ya uchaguzi kuona kwamba wanatekeleza haki ya demokrasia ya kuchaguwa viongozi wao,” alisema.

Pia alisema kwamba utaratibu wa maandalizi ya kura ya mapema ambayo itapigwa siku moja kabla ya uchaguzi yamekamilika. “Kura ya mapema imeandaliwa kwa mujibu wa utaratibu unaofahamika kwa mujibu wa sheria...kwa hivyo hakuna dosari zitakazojitokeza katika upigaji kura,” alisema.

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Thabit Faina Idarous alisema maandalizi ya Uchaguzi Mkuu yanaendelea vizuri ambapo kazi ya uandikishaji wapigakura pamoja na kuhakiki imekamilika ikiwemo ugawaji wa shahada za kupigia kura.

Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini wamkuwa wakielezea wasiwasi na hofu yao kuhusu kura ya mapema itakayopigwa siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi