loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais wa zamani Mexico kizimbani kwa ufisadi

WAENDESHA mashitaka nchini Mexico wameanzisha uchunguzi wa rushwa na ufi sadi dhidi ya Rais wa zamani wa nchi hiyo, Enrique Peña Nieto.

Hatua hiyo inatokana na Mkuu wa zamani wa kampuni ya nishati ya serikali, Emilio Lozoya kumtuhumu Nieto kuchukua mamilioni ya dola kwa rushwa kuwahonga wabunge.

Lozoya aliondolewa Hispania mwezi uliopita ili kusomewa mashitaka ya tuhuma za rushwa yaliyohusisha pia mradi mkubwa wa ujenzi wa Brazil wa Odebrecht.

Nieto aliyekuwa madarakani kuanzia mwaka 2012 hadi 2018 hajasema lolote.

Mwaka jana mashuhuda walitoa ushahidi katika kesi ya Marekani inayomhusu anayedaiwa kuwa mfanyabiashara mkubwa wa dawa za kulevya, Joaquin "El Chapo" aliyedai kuwa Nieto alikubali Dola za Marekani milioni 100 kama rushwa kutoka kwa genge la wauza dawa za kulevya.

Nieto hakusema chochote kuhusu tuhuma hizo, lakini awali alikana kuhusika na rushwa.

 

JUMUIYA ya Nchi za Afrika, Carribean na Pacifi c (OACPS) ...

foto
Mwandishi: MEXICO CITY, Mexico

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi