loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwandishi Wetu

BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na uongozi wa Wilaya ya Nanyumbu, wamekubaliana kujenga ghala la kuhifadhi tani 5,000 za korosho wilayani humo kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo (SCGS).

Aidha kazi hiyo itafanyika kwa ushirikiano na Chama Kikuu cha ushirika cha Masasi and Mtwara Cooperative Union (MAMCU).

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazungumzo hayo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Moses Machali, alisema ghala hilo litatatua tatizo la hifadhi korosho wilayani humo na kuwaondolea usumbufu wakulima.

“Mipango ya TADB ni kuleta mageuzi makubwa katika kilimo ili kwenda sambamba na sera ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ya kujenga uchumi wa viwanda.

Malighafi ni moja ya vitu muhimu na mazao ndiyo malighafi muhimu za viwanda vyetu. Tutajitahidi iwezekanavyo kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo ili kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa pato la faifa,” alisema Justine.

Korosho ni kati ya mazao manane yanayotambuliwa na serikali kuwa ni mazao ya asili ya biashara. Korosho sasa limefanywa kuwa zao la kimkakati kuinua pato la wakulima na kuendeleza ajenda ya taifa ya uchumi wa viwanda.

Uzalishaji wa korosho umekuwa ukiongezeka kila mwaka kutoka tani 155,416 msimu wa kilimo wa 2015/16 hadi zaidi ya tani 350,000 msimu 2018/2019.

TADB kupitia mfuko wa dhamana kwa Wakulima Wadogo kwa kushirikiana Chama cha Ushirika cha Masasi na Mtwara (MAMCU) imefadhili ujenzi huu wa ghala lenye uwezo wa kuhifadhi tani 5,000 za korosho wilayani Nanyumbu.

Kwa mujibu wa bosi huyo wa Benki ya Maendeleo ya Wakulima Tanzania, hatua hii itapunguza gharama na kumpa unafuu ya gharama za usafirishaji mkulima.

Aliwataka wakulima wajivunie TADB kwa kuwa ni yao na benki hiyo itatoa ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu ya uzalishaji wa mazao kuanzia namna ya kuandaa mashamba, upatikanaji wa madawa sahihi, usafirishaji pamoja na uhifadhi wa mazo mpaka uzalishaji uwe marudufu au zaidi.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi