loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Geita Gold Mining yasaini mpango kusaidia jamii bil 9/-

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) pamoja na Halmashauri ya Mji wa Geita zimesaini makubaliano ya utekelezaji wa Mpango wa Kusaidia Jamii (CSR) kwa mwaka 2020 wenye thamani ya Sh bilioni 9.2.

Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Richard Jordinson alisema hatua hiyo inatekeleza malengo ya kampuni hiyo kuendeleza ushirikiano na serikali za mitaa na jamii nzima kwa ujumla katika kutambua na kusimamia miradi muhimu kwa mustakabali endelevu wa mkoa wa Geita.

“Tunafurahi kuendeleza ahadi yetu kwa serikali na jamii ya wenyeji. Katika mwaka huu wa tatu wa utekelezaji wa mpango huu baada ya mabadiliko ya sheria ya madini, ni matumaini yetu kuwa tunaweza kuendeleza tulipoishia katika miradi iliyopita ili kuongeza tija na umiliki kwa jamii.

“Tangu GGML ianzishwe, imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na serikali ya Mkoa wa Geita kusaidia miradi kadhaa ya kijamii katika mkoa huo kupitia ushirikiano baina ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP) sanjari na Mpango ya Kitaifa.

“Pamoja na tunu yake kuu ya kusaidia jamii ya Geita kuwa na maendeleo endelevu kijamii na kiuchumi ambayo yatabakia hata baada ya shughuli za uchimbaji kumalizika, pia kampuni imefadhili utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwamo usambazaji wa maji safi, uendelezaji wa shughuli za uchumi katika sekta za kiimo, ujenzi na huduma,” alisema.

Makubaliano hayo sasa yamethibitisha ahadi ya GGML kwa serikali baada ya kutekeleza mabadiliko yaliyomo kwenye kifungu cha 105 cha Sheria ya Madini ambacho kinajumuisha utekelezaji wa Mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

Utekelezaji wa mpango huo utanufaisha jamii ya Geita katika maeneo ya mazingira, miundombinu, afya, elimu na biashara ndogo na za kati.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi