loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

FARID ATUA JANGWANI, AZAM NAO WAFANYA YAO

KLABU ya Yanga imetangaza kumsajili winga wa kimataifa wa Tanzania Farid Mussa kwa mkataba wa mwaka mmoja. Winga huyo aliyekuwa akikipiga katika klabu ya soka ya Tenerife ya Hispania amemaliza mkataba wake huko na kujiunga na mabingwa wa kihistoria kama mchezaji huru.

Akizungumzia usajili wa mchezaji huyo jana Msemaji wa Yanga Hassan Bumbuli alisema umetokana na mahitaji, walikuwa wakihitaji winga mwenye kasi na uwezo mzuri.

“Tunaamini Farid ni chaguo sahihi kwa sasa ndani ya timu ya wananchi na tunafurahi kukamilisha usajili wake,”alisema.

Kabla ya kwenda Hispania kucheza soka la kulipwa aliitumikia Azam FC kwa misimu mitatu 2013 hadi 2016 akitokea kwenye kituo cha kulea vipaji cha klabu hiyo na baadaye akajiunga na Tenerife kwa majaribio na kufuzu.

Meneja wa mchezaji huyo Jemedari Said aliliambia gazeti hili jana kuwa kabla ya kusaini kulikuwa na majadiliano marefu baina ya mchezaji na Yanga kwa zaidi ya siku 10 ili kurekebisha mkataba huo. Kwa mujibu wa Jemedari, Farid bado ana ndoto ya kwenda mbali zaidi hivyo, alitaka moja ya kipengele ni kuruhusiwa kuondoka iwapo atapata timu nje ya nchi.

Huyo ni mchezaji wa nane kusajiliwa Yanga mpaka sasa. Wengine ni Shomari Kibwana, Yassin Mustapha, Bakari Mwamnyeto, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Zawadi Mauya, Waziri Junior na Yacouba Songne.

Yanga bado inaendelea na usajili kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao kwa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Uongozi wa klabu hiyo ulipania kufanya marekebisho ya kikosi hicho ili kurudi katika kasi kupigania taji la ligi baada ya kukosa kwa misimu mitatu mfululizo.

Wakati huo huo, Klabu ya Azam FC imesamsajili beki wa kushoto kutoka Mbao Emmanuel Charles kwa mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru. Msemaji wa Azam FC Thabit Zakaria alisema jana kuwa usajili wake ni sehemu ya kuongeza nguvu katika eneo la ulinzi la Azam FC, likiwa ni pendekezo la benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba.

Beki huyo alikuwa na kiwango bora akiwa na Mbao msimu uliopita, akifanikiwa kutengeneza mabao matatu na kufunga mawili. Huo ni usajili wa sita kwenye kikosi cha Azam FC kuelekea msimu ujao, wengine wakiwa ni kipa David Kissu, Awesu Awesu, Ally Niyonzima, Ismail Aziz na Ayoub Lyanga.

MWIGIZAJI maarufu wa tamthilia ya Karma, Wema Sepetu amewaomba radhi ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi