loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Masumbwi kurindima New Vijana

JUMLA ya mapambano 10 yanatarajiwa kurindima katika ukumbi wa New Vijana Social Hall, Dar-es-Salaam, Agosti 29.

Akizungumza na gazeti hili promota wa mapambano hayo Shomari Kimbau kupitia kampuni yake ya Golden Boy Africa alisema mapambano hayo yapo chini ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBRC).

“Tayari nimepata vibali, hivyo wadau wa masumbi wajiandae kupata burudani waliyoikosa kwa kipindi kirefu baada ya michezo kusitishwa kutokana na janga la corona,” alisema Kimbau.

Kimbau alisema pambano la kwanza litakuwa kati ya bondia Pascal Simba na Hamisi Palasuguru, uzani wa heavyweight raundi 10, pambano la pili litakuwa kati ya Maono Ally na Joseph Sinkala, uzani wa welterweight, raundi nane.

Alisema bondia Jongo Jongo atapigana na Bakari Ali, uzani wa heavyweight, raundi nane, Nasser Mafuru atapanda ulingoni kupigana na Mwinyi Mzengela, uzani wa lightweight, raundi 10.

Pia bondia Ramadhani Mzee ‘Bunju Lagga’ ataumana na Hamza Iddy ‘Bagamoyo boy’, uzani wa flyweight, raundi sita na bondia wa kike Ruth Chisale atapigana na Happy Daudi, uzani wa lightweight raundi sita.

Pia Salim Chazama atamvaa Francis Miyeyusho, uzani wa lightweight raundi na mabondia Idrisa Juma Feruzi, Christopha Magambo na Yusuf Bangu wapinzani wao watatangazwa baadaye.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine