loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Gareth Bale bado yupo sana Madrid

MCHEZAJI Gareth Bale ameamua kuendelea kubaki Real Madrid hadi mwanzoni mwa 2022 mkataba wake utakapomalizika, hiyo ni kwa mujibu wa gazeti la The Mirror.

Gazeti hilo limedai Bale ameamua kubakia hadi mkataba wake utakapomalizika hata kama hatacheza licha ya kutokuwa kwenye mipango ya kocha, Zinedine Zidane, huko Bernabeu.

Raia huyo wa Wales aliripotiwa kumwambia Zidane hatacheza pambano la Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City.

The Mirror linadai Bale anajisikia furaha kubaki Hispania na hataondoka katika msimu huu wa majira ya joto.

“Bale yuko hadi 2022 mkataba utakapokwisha na malipo yake yanafanya timu nyingi England kushindwa kumnunua kwani analipwa Euro 600,000 kwa wiki, hakuna timu nyingine Ulaya inayolipa mshahara huo,” lilisema gazeti hilo.

Bale alikuwa anakaribia  kusaini China Super League kwenye klabu ya Jiangsu Suning majira ya joto msimu uliopita, mpango ambao ungemwezesha kupata pauni milioni 1 kwa wiki.

Sasa, Bale anaonekana kubadili mawazo kwa kuamua kubaki Real hata kama hatacheza hadi mkataba wake utakapomalizika Madrid.

Mchezaji huyo hajacheza tangu Juni 22, muda ambao ulikuwa mwanzo wake wa raundi ya 12 ya msimu katika kampeni ya kuwania taji la La Liga.

Hapo ndipo alipokosolewa kwa tabia yake kwenye benchi kwani alijifanya amelala wakati akitumia barakoa ya uso wake kama kinyago cha macho.

Katika mchezo mwingine alijifanya uso wake ulikuwa darubini na akatazama mchezo huo kupitia miguu yake juu ya viti.

Hata hivyo, licha ya kuvunjika kwa uhusiano wake na wakuu wa Madrid, Bale anaonekana amedhamiria kusubiri mkataba wake umalizike ndipo aondoke mwaka 2022.

LIVERPOOL inakaribia kumsajili kiungo ...

foto
Mwandishi: MADRID, Hispania

Post your comments

Habari Nyingine