loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wizara yaagiza maeneo kupimwa

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba, na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula (pichani) ameziagiza idara za ardhi kwenye halmashauri zihakikishe maeneo yanayotengwa kwa ajili ya uwekezaji yanapimwa na kuwe na mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye vijiji.

Dk Mabula alisema hayo wilayani Bukombe jana wakati akiwa katika ziara ya kikazi kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi sanjari na kukagua miradi inayejengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani Geita.

Alisema, kuna maeneo kwenye baadhi ya halmashauri yametengwa kwa ajili ya shughuli za uwekezaji lakini hayajapimwa na pia baadhi ya vijiji havina mipango ya matumizi bora ya ardhi.

Kwa mujibu wa Dk Mabula, wakati wa mchakato wa kutenga maeneo ya uwekezaji ndani ya halmashauri, ni vizuri utengaji maeneo ukaenda sambamba na kuyapima na pia juhudi ziongezwe kuviwekea vijiji mipango ya matumizi bora ya ardhi.

Katika ziara hiyo, Dk Mabula alitembelea pia halmashauri za Wilaya za Chato na Geita na kuziagiza ziongeze kasi katika uwekeji mipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji sanjari na kuvipatia hati ili kuondokana na migogoro ya mara kwa mara hasa ya wakulima na wafugaji.

Wakati akiwa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, alielezwa kuwa halmashauri kwa kushirikiana na timu ya mpango wa matumizi bora ya ardhi taifa imeandaa na kutekeleza mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye vijiji vitano vya Kagwe, Kidete, Bukombe, Ilalwe na Nasihukulu.

JAMII imehadharishwa dhidi ya tabia ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalum,

Post your comments

Habari Nyingine