loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ukimwi waua wanaume zaidi kuliko wanawake

WANAUME wanasemekana kuathiriwa zaidi na maradhi ya Ukimwi, ikilinganishwa na wanawake.

Utafiti uliofanywa na Idara ya Afya katika Wizara ya Afya nchini Kenya, umeonesha kuwa, asilimia 51 ya wagonjwa wanaofariki kutokana na magonjwa yenye uhusiano na Ukimwi ni wanaume.

Utafiti huo umeonesha kuwa, wanaume 13,800, ikilinganishwa na wanawake 10,100, wanapoteza maisha kwa mwaka, ikiwa ni jumla ya wagonjwa 28,200.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, nchini Kenya wanaume 523,600 na wanawake 864,600 wanaishi na virusi vya ugonjwa huo.

Takwimu hizo zimeshangaza kuona wanaume wanaongoza kwa kuwa na wagonjwa wachache wa ukimwi, lakini ndio wanaongoza kwa vifo.

Utafiti huo umeonesha moja ya mambo yanayosababisha wanaume kupoteza maisha kwa wingi ni tabia ya kutofuatilia taratibu za afya pindi wanapogundua kuwa wameathirika.

Mambo mengine ni ulevi wa kupindukia unaosababisha wanaume kushindwa kuzingatia mlo kamili unaomarisha kinga ya mwili na tabia za kimila ambazo zinawabeba zaidi wanaume kuliko wanawake.

Wanaume pia wamekuwa wakiendekeza ngono zembe mara kwa mara badala ya kuzingatia ushauri wanaopewa katika kliniki wanakopatiwa matibabu na ushauri.

Kwa upande mwingine, wanawake wamekuwa wastaarabu katika kuzingatia taratibu za afya, ikiwamo  kutumia dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi na matumizi sahihi ya mlo kamili.

FAMILIA 5,000 katika mji mkuu wa ...

foto
Mwandishi: NAIROBI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi