loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hati za kusafiria za Rwanda mwisho Juni 28

HATI za kusafiria za Rwanda hazitatumika ifikapo Juni 28, mwakani, baada ya nchi hiyo kuanza kutumia hati za kusafiria za kielektroniki za Afrika Mashariki Juni, mwaka jana.

Taarifa ya Idara ya Uhamiaji iliyotolewa juzi kwa vyombo vya habari, ilisema hati zote za kusafiria zilizotolewa kabla ya Juni 27, 2019 zitaondolewa kwenye matumizi na nafasi yake kuchukuliwa na hati ya kusafiria ya kielektroniki za Afrika Mashariki. 

Baada ya nchi hiyo kutoa hati hizo za kidijiti, wamiliki wa hati za zamani walipewa miaka miwili kubadilisha na kupata mpya.

Hati hizo mpya pia zinatumiwa na nchi nyingine za EAC zikiwamo Tanzania, Kenya na Uganda na zinakubalika duniani kote.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa, hati hiyo mpya inatoa fursa kwa msafiri kuingia katika nchi mbalimbali bila kuhitaji visa.

Alisema baada ya muombaji kufanya malipo ya kupatiwa hati mpya ya kusafiria, atapokea ujumbe mfupi wa maneno unaomtaka kufika idara ya uhamiaji akiwa na picha zake kwa ajili ya kuchukuliwa alama za vidole.

FAMILIA 5,000 katika mji mkuu wa ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi