loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mradi uboreshaji elimu wapata mafanikio

UTEKELEZAJI wa mradi wa utoaji elimu bora kwa maendeleo ya watu awamu ya kwanza umefikia asilimia 81 kwa ujenzi wa madarasa ya kawaida, asilimia 85 kwa ujenzi wa vyoo na asilimia 45 kwa ujenzi wa majengo ya shule ya ghorofa mbili.

Aidha, Wizara ya Elimu imesema maendeleo ya mradi huo awamu ya pili ambayo imeanza nchi nzima kwa sasa ni asilimia 14.

Mtaalamu wa masuala ya elimu, habari na mawasiliano katika wizara ya elimu, Flavia Salafina, juzi alisema ujenzi huo umefadhiliwa na Benki ya Dunia na serikali.

Alisema katika kukabiliana na msongamano wa wanafunzi na kusafiri kwa muda mrefu wakati wa kwenda shule na kurejea nyumbani, wizara hiyo imesema imepanga kujenga vyumba vya madarasa 22,505 Juni, mwaka huu. 

Alisema mradi huo unatarajiwa kutekelezwa katika wilaya zote 30 kufikia Septemba, mwaka huu.

Kwa mujibu wa wizara ya elimu, ujenzi huo unafadhiliwa na serikali kwa thamani ya faranga bilioni 96.4, huku Benki ya Dunia ikitoa mkopo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 200 (sawa na faranga bilioni 180).

Ilisema dola za Marekani milioni 126 zimetolewa kwa ajili ya kupunguza msongamano darasani na fedha zilizobaki zimeelekeza katika shughuli nyingine ikiwamo mafunzo kwa walimu na ujenzi wa vyuo vya walimu.

FAMILIA 5,000 katika mji mkuu wa ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi