loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga yanasa mbadala wa Morisson

KLABU ya Yanga imesema inatarajia kumsajili Carlos do Carmo ‘Carlinhos’ kuziba nafasi ya kiungo, Bernard Morrison aliyesajiliwa na Simba.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi  wa Uwekezaji- GSM ambao ni wadhamini wao, Hersi Said na kusema baada ya kukamilisha usajili wa wachezaji Mukoko Tonombe na Tuisila Kisinda kutoka AS Vita Club ya DR Congo sasa wanahamia kwa washambuliaji.

Alisema baada ya kumleta Carlinhos wanatarajia kumleta mshambuliaji ambaye aligoma kumtaja jina lake kwa sababu bado hawajafanya mazungumzo na timu anayoichezea ili kujiunga na Yanga kwa msimu ujao.

“ Tunatarajia kumaliza usajili wa Carlinhos, raia wa Angola anayekuja kuziba nafasi ya Morrison na mwingine siwezi kumtaja kwa kuwa bado ana mkataba na timu yake na hatujakamilisha mazungumzo, tuwe na subira,“ alisema Said.

Alisema mara baada ya kukamilisha usajili, watamtangaza mchezaji huyo na watasaidia kuunda kikosi kitakachotoa ushindani kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano mengine.

Pia alisema wanatarajia kumtangaza kocha mkuu kesho au kesho kutwa kama mazungumzo yao yanayoelekea mwishoni yatakwenda sawa na kukubaliana.

TIMU ya soka ya Mtibwa Sugar imesema mchezo ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi