loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mradi kusaidia walioathirika na majanga wazinduliwa

WIZARA ya Usimamizi wa Majanga imezindua mradi wa miezi sita wenye thamani ya dola za Marekani milioni moja kwa ajili ya kusaidia wananchi walioathirika na majanga katika wilaya za Nyabihu, Ngorororero  na Gakenke. 

Fedha za mradi huo wa ‘Provision of Emergency Shelter and Agriculture Support to Communities Affected by Floods and Landslides in Rwanda’, zimetolewa na serikali ya Rwanda. 

 “Sekta za afya, kilimo, nyumba miundombinu na mazingira zimeathirika kwa kiwango kikubwa kwa takwimu zilizokusanywa kutoka wilaya zote 30 zilizokumbwa na majanga hayo,” ilisema wizara hiyo.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, watu 317 walikufa, nyumba 8,143 ziliziharibiwa kabisa au kubomoka baadhi ya sehemu na hekta 9,383 za mazao ziliharibika, pamoja na madhara mengine kutokana na majanga hayo.

Ripoti hiyo ilisema wilaya tatu ziliathirika vibaya kwa mafuriko na maporomoko kuanzia Septemba 2019 mpaka Mei, mwaka huu kutokana na  mvua kubwa nchini humo.

Wizara ya maafa ilieleza kuwa, mradi huo unalenga kusaidia kaya 2,900 zenye watu 13,651ambazo zimeathirika, ambapo zitasaidiwa zana za kilimo kama majembe, vifaa vya umwagiliaji na uboreshaji mbegu kwa dola za Marekani 200,000.

Aidha, kaya 1,765 zenye watu 7,027, zitasaidiwa misumari, saruji, mabati, nyaya na vifaa vingine vya ujenzi kwa dola za Marekani 800,000.

FAMILIA 5,000 katika mji mkuu wa ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi