loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Akiba ya fedha mfuko wa uwekezaji yaongezeka

AKIBA ya fedha katika Mfuko wa Taifa wa Uwekezaji Rwanda Iterambere (RNIT), imeongezeka kwa asilimia 32 kutoka faranga bilioni 10.91 kuanzia Desemba, mwaka jana mpaka Julai, mwaka huu.

Mpaka Julai mwaka huu, mapato yaliyotoka moja kwa moja kwa wawekezaji 5,000 wenye wanachama zaidi ya 24,200 kutoka vyombo mbalimbali na taasisi tisa za uwekezaji.

Mfuko wa Iterambereni ulizinduzliwa Julai, 2016 na kufikia Desemba, 2017 ulikuwa umekusanya zaidi ya faranga bilioni 1.464 na imekuwa ukikua kwa kasi na kupata faida ya mwaka kutoka asilimia 9.77 mwaka 2017, mpaka asilimia 10.76, mwaka huu.

Mtendaji Mkuu wa kampuni ya RNIT inayosimamia mfuko huo, Jonathan Sebagabo, alisema awali walikuwa na hofu ya ugonjwa wa covid-19 kwamba ungesababisha wanachama kutoa fedha nyingi na kuathiri ukuaji wake.

Alisema kiwango kikubwa cha fedha hutolewa Januari wakati wanafunzi wanarejea shule na wazazi kulazimika kulipa ada kwa watoto wao au katika matukio ya sherehe za mwaka mpya.

“Tulikuwa na hofu kuwa, watu watachukua akiba zao hivyo kuathiri mfuko, lakini ingawa walitoa baadhi ya akiba zao kukidhi mahitaji yao, mfuko umeendelea kukua, jambo linaloonesha watu wanaelewa umuhimu wa kuweka akiba na kazi ya mfuko ni kusaidia kukabili matatizo ya kiuchumi ya wanachama wake,” alisema.

FAMILIA 5,000 katika mji mkuu wa ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi