loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uporaji ardhi washamiri Juba

WAZIRI wa Ardhi na Nyumba, Michael Chiangjiek, amesema uporaji wa ardhi umeshamiri katika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba.

Akizungumza na Radio Tamazuj ya nchi hiyo jana, alisema wizara yake inasubiri kuundwa kwa serikali za majimbo ili iweze kuweka mipango ya pamoja ya kukabiliana na suala hilo.

"Kuna matatizo mengi yanayoendana na uporaji ardhi katika maeneo ya Mangatain, Gumbo Sherikat na ya jirani, tunasubiri kutangazwa kwa serikali ya jimbo la Central Equatorial ili kueleza mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo.” 

 “Nimepokea kesi nyingi kuhusu uporaji ardhi, migogoro na upangaji wa ardhi, lakini wizara hatuwezi kufanya kazi bila serikali ya jimbo husika ili kutatua migogoro iliyopo,” alisema.

Kwa mujibu wa Chiangjiek, wizara hiyo inaendelea na mpango wa kukabiliana na tatizo hilo katika maeneo jirani ambayo hayatafanyiwa utafiti.

Alisema uporaji ardhi umekuwa ukisababisha matatizo mengi katika jamii za watu wa Juba, lakini watu waliopeleka malalamiko ya kuchukuliwa ardhi zao itabidi wasubiri mpaka kuundwa kwa serikali mpya ili kupata ufumbuzi.

Alisema kuna kesi mbalimbali zilizopo mahakamani zinazohusu masuala ya ardhi, ambapo katiba ya mpito inaeleza kuwa, ardhi yote ya nchi hiyo inamilikiwa na raia wa Sudan Kusini, gharama za umiliki wa ardhi, matumizi yake na haki ya kumiliki.

FAMILIA 5,000 katika mji mkuu wa ...

foto
Mwandishi: SUDAN KUSINI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi