loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pauni ya Sudan yaporomoka thamani

SERIKALI imetangaza kuongeza fedha za kigeni katika mzunguko, baada ya pauni ya nchi hiyo kuvunja rekodi  kwa kushuka thamani kwa kiwango kikubwa dhidi ya Dola ya Marekani katika masoko yasiyo halali.

Akizungumza na vyombo vya habari mjini Juba juzi, Naibu wa Pili wa Gavana wa Benki Kuu, Kech Pouch, alisema uzalishaji wa mafuta umeshuka kutokana na ugonjwa wa covid-19 hivyo kusababisha upungufu wa fedha za kigeni.

“Ni vigumu kwa sasa kudhibiti ongezeko la kiwango cha kubadilisha fedha kwa sababu hatuna rasilimali na hatuna  akiba ya kutosha ya fedha za kigeni,” alisema.

Sudan Kusini inapata kiwango kikubwa cha mapato yake ya kigeni kutokana na mauzo ya mafuta, lakini kwa sasa imekuwa ikitoa mapipa ya mafuta ghafi 180,000 kwa siku kutoka mapipa 250,000 kabla ya mlipuko wa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013.

Pouch alisema nchi hiyo ina maeneo matatu ya kubadilisha fedha, ambavyo ni benki za biashara, Benki Kuu na masoko yasiyo rasmi.

Katika Benki Kuu pauni 165 zinabadilishwa kwa dola moja, huku katika benki za biashara pauni 190 zikibadilishwa kwa dola moja na katika masomo yasiyo halali pauni 400 kwa dola moja.

Hata hivyo, alisema mfumuko wa bei umebaki asilimia 35 kutokana na kushuka kwa kiwango kikubwa thamani ya pauni ya nchi hiyo. 

Alisema mwaka 2016 mfumuko wa bei ulifikia asilimia 800 na kusababisha nchi hiyo kukabiliwa na baa la njaa.

FAMILIA 5,000 katika mji mkuu wa ...

foto
Mwandishi: JUBA

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi