loader
Mgombea ubunge Mtama mbaroni kwa tuhuma za rushwa Lindi 

Mgombea ubunge Mtama mbaroni kwa tuhuma za rushwa Lindi 

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Lindi imemkamata mgombea ubunge Jimbo la Mtama kwa tiketi ya Chadema, Suleiman Mathew kwa tuhuma za kutoa rushwa ya 1,540,000/- kwa afisa uchaguzi.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa nia ya kutoa kiasi hicho kwa Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtama ni kushawishi kusaidiwa atangazwe  mshindi.

Mkuu wa  TAKUKURU mkoani hapa,  Stephen Chami amewaambia wanahabari  ofisini kwake kwamba mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo, Jumanne (Agosti 25, 2020).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mtuhumiwa huyo alikamatwa Jumatatu (Agosti 24, 2020) akitoa rushwa kwa afisa uchaguzi pamoja na msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Mtama mama kishawishi ili aweze kusaidiwa kutangazwa mshindi wa  nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Mtama mara baada ya upigaji kura kukamilika.

"Taarifa inaeleza kuwa ili kutimiza lengo lake la kutangazwa kuwa mshindi, yeye aliandaa jumla ya Sh milioni 10 kwa ajili ya kuwapa wote wawili ili wamsaidie kutangazwa mshindi katika nafasi ya ubunge," alisema Chami.

foto
Mwandishi: Anne Robi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi